Matajiri wa dhababu Geita Gold tayari wameanza kujiimarisha kimyakimya kuelekea msimu ujao ambao watashiriki katika michuano ya Kimataifa na Ligi ya ndani.
Geita Gold imeanza na eneo la kiungo huku usajili huu ukiwa mahususi kwaajili ya mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika wakianza na eneo hilo muhimu la uwanja.
Ramadhani Chombo “Redondo” inasemekana tayari ameshamalizana na matajiri wa dhababu Geita Gold akiwa mchezaji huru kutokea Biashara Utd iliyoshuka daraja.
Si tu Ramadhan Chombo mchezaji wa zamani wa Simba na Mbeya City lakini pia Geita imefanikiwa kupata saini kiungo fundi wa Polisi Tanzania Deusdedity Okoyo na mlinzi wa zamani wa Simba, Mbeya City na Lipuli fc Haruna Shamte.
Geita ambayo kwa mara ya kwanza imecheza Ligi Kuu msimu uliomalizima na kukata tiketi ya kwenda katika michuano ya Kimataifa imedhamiria kufanya vyema katika michuano hiyo kwa kusajili wachezaji wazoefu.