Klabu ya soka ya Yanga imefanikiwa kutwaa na kutetea taji lao la kombe la FA baada ya kuifunga Azam Fc kwa bao moja bila katika uwanja wa Mkakwani.
Bao la Kenedy Musonda katika dakika ya 12 akiunganisha krosi ya Djuma Shaban ndio liliamua mchezo huo uliohudhuriwa na mashabiki wengi wa soka waliojitokeza katika uwanja wa Mkwakwani.
Baada yakutwaa kombe hilo sasa Yanga kwa msimu huu imefanikiwa kutwaa mataji mataji matatu (Ngao ya Jamii, Ligi Kuu ya NBC na kombe la FA) huku wakilikosa kombe la Mapinduzi na Kombe la Shirikisho Afrika walilomaliza katika nafasi ya pili.
Vikosi vilivyokua katika mchezo wa leo
Kikosi cha Azam Fc kinachoanza!
1. Idrissa Abdoulae
2. Lusajo Mwaikenda
3. Bruce Kangwa
4. Abdalla Kheri
5. Daniel Amoah
6. Issa Ndalla
7. Abdul Sopu
8. Sospeter Banyana
10. James Akamiko
11. Lyanga Ayoub
Sub: Masoud, Manyama, Idd Nado, Msindo, Chilambo, Dube, Mkandala, Tepsi na Kipre Jnr.
Mfumo 4:2:3:1
Kikosi cha Yanga kinachoanza!
1. Djigui Diarra
2. Djuma Shaban
3. Joyce Lomalisa
4. Ibrahim Bacca
5. Bakari Mwamnyeto
6. Dickson Job
7. Sure Boy
8. Khalid Aucho
9. Kenedy Musonda
10. Benard Morrison
11. Tuisila Kisinda
Sub: Metacha, Kibwana, Bryson, Doumbia, Mauya, Nkane, Mudathir, Bangala, Mzize
Mfumo 3:5:2
Matukio muhimu katika mchezo huo!
1′ Mpira umeanza hapa katika Dimba la Mkwakwani Tanga.
12′ Gooaaaaaal Kenedy Musonda anaipa uongozi Yanga hapaa Mkwakwani.
39′ Kadi ya njano kwa Dickson Job baada ya kumchezea madhambi mshambuliaji Ilunga Mbombo
45+3 Mpira ni mapumziko, Yanga wanakwenda mapumziko wakiwa mbele kwa bao moja kwa sifuri.
45′ mpira umeanza tena kwa kipindi cha pili Mkwakwani.
45′ Prince Dube anaingia kuchukua nafasi ya Issa Ndalla
60′ Kipre Jnr anaingia kuchukua nafasi ya Ayoub Lyanga na Bruce Kangwa anatoka kumpisha Pascal Msindo
77′ Mabadiliko Benard Morrison na Salum Aboubacar wanatoka na nafasi zao zinachukuliwa na Yanick Bangala na Clement Mzinze.
86′ Kenedy Musonda anapata kadi ya njano baada ya kumfanyia madhambi James Akamiko
90′ zimekamilika na mwamuzi anaongeza dakika 9 hapa Mkwakwani.
90+2 Anatoka Djuma Shaban anaingia Kibwana Shomary, anatoka Sospeter Banyana anaingia Idd Nado
90+8 mpira umemalizika hapa Mkwakwani