Baada ya kufanikiwa kuivusha Yanga Sc kwenda fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika mshambuliaji Fiston Mayele amekiri huu ndio msimu wake bora tangu aanzw kucheza soka.
Mayele katika mchezo wa nusu fainali dhidi ya Singida Big Stars aliingia katika kipindi cha pili na kufunga bao pekee lililowapeleka fainali Yanga fainali ambapo watacheza na Azam Fc na baada ya mchezo kumalizika Mayele amesema
“Huu ndio msimu bora kwangu naweza nikasema hivyo, sikuwahi kufunga mabao saba katika michuano ya CAF ni kwa mara ya kwanza katika maisha yangu ya soka.
Hii inaonyesha ni msimu bora sana kwangu mimi kwahivyo namshukuru sana Mungu, na naomba niendelee hivi mpaka mwisho wa msimu.”
Mpaka sasa Fiston Mayele amefunga mabao mawili katika michuano ya FA, mabao saba katika Kombe la Shirikisho Afrika huku akiwa na mabao 16 katika Ligi Kuu ya NBC. Mpaka saza Yanga wamebakiza michezo miwili ya Ligi Kuu, mchezo mmoja wa fainali ya FA na michezo miwili ya fainali ya Shirikisho.
Kuelekea mchezo wa fainali ya FA ambao utapigwa mkoani Tanga katika Dimba la Mkwakwani Fiston Mayele amekubali wanakwenda kukutana na mchezo mgumu kutokana na tabia za wachezaji wa Azam Fc wanapokutana na timu kubwa.
“Fainali utakua mchezo mzuri na mgumu, Azam wana timu nzuri na wanawachezaji wazuri ambao wanakamia sana mechi kubwa, wakicheza na Yanga au Simba ndio unawaona.
Lakini ukienda kuangalia wakicheza na Namungo ama timu zingine wale wachezaji utawasahau, kwaiyo tunajua tunakwenda kucheza fainali ngumu dhidi ya Azam kwasababu tunakwenda kucheza na timu ngumu yenye wachezaji wazuri na wanaojua kukamia mechi kubwa,’ alimaliza Mayele.