Kamati ya nidhamu ya Shirikisho la Kandanda Ulimwenguni (FIFA), limetangaza kumfungia maisha aliyekuwa Makamu wa Rais wa shirikisho la Kandanda nchini (TFF) Michael Richard Wambura.
Katika barua ya FIFA iliyosainiwa na naibu katibu mkuu wa kamati ya Nidhamu Julien Deux na nakala kutumwa Shirikisho la Kandanda Afrika, kifungo hicho kinamfanya Wambura kutojihusisha na soka maisha.
Hukumu hiyo ya kamati ya maadili ya FIFA inaelezwa kukazia ile hukumu ya kamati ya rufaa ya TFF iliyokuwa chini ya Mwenyekiti wake Marehemu Hamidu Mbwezeleni ambayo Wambura licha ya kuwa Makamu Mwenyekiti wa TFF, hakutakiwa kujihusisha na soka.
Hukumu ya TFF ilitolewa April 6, 2018 na katika
barua hiyo ya FIFA imesema“ Bwana Wambura amefungiwa kutojiuhusisha na soka
duniani kote kwa maisha yake yote, kwa mujibu wa kamati ya maadili ya Tanzania,
Hukumu hii inahusisha majukumu yote ya mpira wa miguu yanayosimamiwa na FIFA na
washirika wake,”