Sambaza....

Baada ya kuishuhudia timu yake ya zamani Manchester United ikimaliza ukame wa miaka sita katika uwanja wa Wembley Sir Alex Fergison amesema bado timu yake inahitaji mshambuliaji mwingine.

Machester United chini ya Eric Ten Hag jana ilifanikiwa kutwaa kombe la Carabao kwa kuifunga Newcastle United kwa mabao mawili kwa bila katika mchezo wa fainali ambao Sir Alex Fergison alikua miongoni mwa mwashuhuda wa mchezo huo Wembley.

 

Katika mchezo huo magoli ya Manchester United yalifungwa na kiungo Mbrazil  Casemiro na Marcus Rashford katika kipindi cha kwanza cha mchezo.

Kocha huyo wa zamani wa United amesema Marcus Rashford ni mshabuliaji hatari lakini sio mchezaji wakumtegemea na kumuachia majukumu yote ya mshambuliaji wa mwisho.

Marcus Rashford akishangilia bao lake lapili dhidi ya Newcastle.

“Sidhani kama ni mshambuliaji. Anashambulia mbali akitokea upande wa kushoto na amekuwa mzuri. Umaliziaji wake umekua mzuri kila mara, hupiga maahuti yake chini,  ambayo ni kitu muhimu sana kwa mshambuliaji. na yuko katika kiwango bora kwasasa.

Kwa bahati mbaya kwetu yeye ndiye chanzo kikuu cha magoli, tunaweza kutafuta mshambuliaji mmoja wa ziada, lakini (Rashford) anafanya vyema kwenye kufunga” Alex Fergison

Mpaka sasa Marcus Rashford ameifungia Machester United mabao 25 katika michuano yote na magoli matatu katika timu yake ya Taifa England katika kombe la Dunia.

Sambaza....