Nilijikuta nakumbuka kitabu cha simulizi za kipelelezi kilichotungwa na A. Musiba akimtumia muhusika mkuu Willy Gamba nyakati hizo, kikiitwa “HOFU”.
Kitabu kizuri cha kusisimua kwa wale wapenzi wa simulizi za aina hiyo mimi nikiwa miongoni mwao.
Lakini katika lugha ya adhimu ya Kiswahili ‘HOFU’ ni woga au mashaka ama kutokuwa na utulivu wa jambo yawezekana nafasi yako unayoishikilia huenda ukawa na hofu ya kutwaliwa na mwingine ana taarifa zako unahofu kuvuja.
Lakini pia huwa na kitu cha kiimani zaidi juu ya ‘Hofu’ ya Mwenyezi Mungu juu ya makatazo na maangalizo kama muongozo wa maisha ya binadamu huku duniani
Mie nipo kwenye’ hofu’ ya kutwaliwa kwa nafasi unayoimilikia au kuishikilia na mtu.
Wote tukakubaliana ‘gumzo kama si homa jiji’ kwenye soko la usajili ni Stephane Aziz Ki raia wa Bukinafaso ‘anayeupiga mwingi’ pale Asec Mimosa Ivory Coast.
Anatajwa sana kujiunga na vilabu vikubwa viwili vya nchini Tanzania Simba na Yanga.
Huku Yanga maarufu kama ‘Wananchi ‘wakiwa na 99% ya kumpata na yawezekana washampata.
Kama ndivyo ile dhana ya ‘hofu’ ndiyo inaingi hapa kwa wachezaji wa sasa ndani ya Yanga hasa wale wa safu ya ushambuliaji ama waweza kusema mstari wa mbele.
Jamaa ni fundi haswa kwa uwezo aliouonesha katika kombe la shirikisho lakini historia ya mapito yake kisoka hadi sasa kuna jambo la kujifunza.
Huyu ni mchezaji anayetumia mguu wa kushoto watangazaji wa zamani wazee wetu watakuambia’ guu la kushoto ama mashoto’ kukutisha zaidi na kutia nakshi simulizi zao.
Nafasi anazozimudu ni zote za mstari wa mbele lakini ni mtamu zaidi akicheza 7,8 10 na 11kifupi ni’ Attacking midfielder ‘ au waweza kusema ni kiungo mshambuliaji.
Na hapo ndiyo hofu inapotanda ndani ya kikosi cha kwanza cha Yanga au Wananchi kama wanavyopenda kujiita wenyewe.
Nani atapoteza namba yake ili kumpisha huyu fundi wa Kibukinabee ? Mayele nina uhakika si mwathirika wa moja kwa moja wa ujio wa Aziz Ki.
Tukiwaangalia wale wanaocheza nafasi za kushabihiana, hatma zao zikoje vip Fei Toto hana hofu umejiuliza Moloko kule winga ya kulia umewahi kufikiri Sure boy, Faridi, Ngushi na dogo Nkane, Kaseke naye ndiyo safari yake itabarikiwa na ujio wa huyu jamaa ni kweli utulivu upo kwa hawa wachezaji kwa sasa?
Mimi naamini kupitia uzoefu wangu wa mchezaji mwenye uwezo wa jamii hii unaibua hofu kubwa sana miongoni wa wachezaji waliopo.
Nimalizie kwa kusema Aziz Ki karibu Tanzania uwazindue waliolala Fei hakupaswa kuwa na hofu ile wewe ulipaswa kuwa na hofu kama si kupishana uwanja wa ndege siku unafika yeye anaondoka kwenda kule Ulaya ulikoshindwa wewe.