Mwezi wa pili tayari umeanza na kwa watu wa Kandanda haswa kandanda la Afrika ni mwezi wa Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho baada ya kukosa burudani hiyo tangu mwaka jana.
Kwa upande wa Simba ambao wanaaminika ndio timu yenye mafanikio zaidi katika soka la Kimataifa nchini watakua na vibarua vizito ambavyo vitaamua hatma yao msimu huu.
Katika mwezi wa pili Simba itakua na jumla ya michezo sita, ikiwepo ya Ligi Kuu ya NBC, Klabu bingwa na mchezo wa kirafiki wa Kimataifa. Katika michezo hiyo sita, Simba itakua na michezo minne ya Kimataifa na miwili pekee ya michuano ya ndani.
Simba itaanza na mchezo wa kirafiki wa Kimataifa February 5 dhidi ya Al-Hilal kutoka Sudan halafu watasafiri mpaka Guinea kucheza mchezo wakwanza wa makundi wa Ligi ya mabigwa dhidi ya Horoya katika mchezo wa kundi D.
Baada ya hapo itarudi nyumbanina baada ya wiki itakua Benjamin Mkapa February 18 dhidi ya Raja Casablanca kisha watapumzika kidogo hapa nyumbani na mchezo dhidi ya Azam Fc.
February 25 Simba watakua wakiwakaribisha Vipers kutoka Uganda mchezo ambao utapigwa Dar-es-salaam katika Dimba la Benjamin Mkapa.
Michezo yote sita (miwili ya ndani) ni muhimu kwa Simba katika kuamua mbio zao za ubingwa dhidi ya Yanga lakini pia michezo mitatu ya Kundi D itaamua kama watafuzu tena na kwenda robo fainali ya Ligi ya Mabingwa.