Sambaza....

Mechi tatu zote ambazo Simba imecheza kuanzia Simba Day dhidi ya Power Dymos, Ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC mpaka fainali yao waliyoshinda dhidi ya Young Africans nimemuangalia vizuri sana Fabrice Ngoma kwa dakika zote alizocheza.

Kwanza kabisa huyu ni “Top Midfilder” kwa ukanda wetu huu wa Afrika Mashariki na Kati kama sio Bara la Afrika. Kuanzia AS Vita Club mpaka Raja Casablanca pale Morocco watu waliona miguu yake ikitoa kitu bora sana ndani ya Uwanja.

 

Ana uwezo wa kucheza kama kiungo mkabaji na akakupa kitu bora sana kwenye eneo hilo! Pia utampanga kama kiungo mchezeshaji na atakupa ubora wake katika eneo hilo! Simba inahitaji sana ubora wake kwa msimu huu.

Ngoma ni miongoni mwa viungo wachache ambao waliimbwa sana kwa wakati ule AS Vita Club ya Florent Ibenge inatikisa Barani Afrika. Sio muda mrefu ni juzi tu 2019 hapo! Baadae akaelekea Al Hilal ya Sudan.

Fabrice Ngoma (katikati) akiitumikia Al Hilal.

Binafsi naona akiwa msaada mkubwa sana ndani ya Simba! Dakika chache alizocheza inaonesha kama akipata muda zaidi na akafanya mazoezi basi miguu yake itafunguka sana na kutoa kitu bora zaidi ya kile ambacho watu wameona mpaka sasa.

Mechi zote tatu mpaka sasa Sadio Kanoute ameanza kikosi cha kwanza lakini baadae Fabrice Ngoma anaingia na kucheza kwa usahihi sana. Bado kuna kitu anacho kwenye miguu yake na atakitoa kadri muda unavyozidi kwenda.

Fabrice Ngoma (katikati)

Rahisi! Fabrice Ngoma kama miguu yake itafunguka zaidi basi naona mmoja atampisha kati ya Kanoute au Mzamiru. Bado majeraha aliyopata kipindi kilichopita yanampa shida kidogo lakini miguu yake ina ubora mkubwa ambao utawalipa Simba hivi karibuni.

Huu ndio ubora ambao Simba SC walihitaji kwenye eneo la kiungo na ubora wenyewe ndio Fabrice Ngoma! Muda utafika na ataonesha kitu iwapo akiwa Ngoma yule wa AS Vita Club basi timu itaimarika kwa kiasi kikubwa sana katika eneo la kiungo.

 

Sambaza....