Walimu wengi wameomba kukinoa kikosi cha Taifa Stars Kwa mujibu wa Oscar Mirambo, Mkurugenzi wa ufundi wa TFF amenukuliwa. Lakini Mtandao wetu unaelewa kuwa Etienne Ndayiragije anaelekea kupata kazi hii baada ya kuisaidia Tanzania kusonga mbele katika mashindano muhimu.
Ingawa hapo mwanzo Shirikisho lilisema kuwa huyu alikuwa kocha wa mpito wakati wakiendelea kumtafuta kocha mpya. Alipewa malengo ya timu, na kwa sasa inawezekana yote yamefikiwa.
Etienne ameisaidia Tanzaia kusonga mbele katika hatua ya Makundi katika kutafuta nafasi ya kufuzu kombe la Dunia, na pia hatua inayofuata katika michuano ya CHAN.
Ukiangalia Stars ya sasa inacheza mpira mzuri wenye malengo, na hii inamaanisha Etienne na benchi lake wameibadili stars, na sasa ipo kimalengo zaidi.
Licha ya kutokupata ushindi ndani ya dakika 90, lakini ameiwezesha timu kufuzu hatua nyingine kwa mikwaju ya penati.
Mirambo amesema kuna orodha ndefu ya makocha ambao wanaitaka kazi hiyo, na Etienne ni mojawapo wa watu wanaoangaliwa na Shirikisho ili kupata nafasi hiyo.
Kwa upande wa Azam, tetesi tulizonazo za chini ya kapeti wameshaanza kujiandaa kwa ajili ya mabadiliko ya benchi la ufundi, na huenda Idd Cheche akaendelea kuinoa klabu hiyo kama safari ya Etienne kwenda Taifa Stars itatimia.
Lakini, Je Etienne yupo tayari kuachana na matajiri wa Jiji, Azam Fc, na kujiunga na timu ya Taifa? Kandanda itakupa jawabu la swali hili.
[poll id=”19″]