Sambaza....

Baada ya sintofahamu ya virusi vya corona na kutokujulikana kwa hatma ya Ligi mbalimbali barani Ulaya,  Vilabu na Mashirikisho ya soka yakijaribu  kutafuta suluhisho ya Ligi zao ni jinsi gani wataweza kumaliza tatizo hilo ni vyema sasa wakageukia nchini China.

Nchini Ubeligiji wao walishakubali msimu huu umekwisha na bingwa ni Club Brugge huku kukiwa hakuna timu itakayoshuka daraja na pia timu mbili tu ndio zitapanda daraja kwa msimu ujao.

Hapa kwetu nchini miongoni mwa Ligi pendwa na zinazofwatiliwa sana ni EPL na Laliga ambazo zimefanikiwa kuteka kiasi kikubwa cha mashabiki hapa kwetu ukiondoa wale wa “Kubet” wanaolazimika kufwatilia Ligi mbalimbali kutokana na kazi yao hiyo.

Kwa kesi hii ya ugonjwa wa corona ni vyema basi FA za Hispania na England wakafiri ni jinsi gani wataweza kuwasiliana na kujenga ujamaa na FA ya China na kuweza kupanga mikakati ambayo itawanufaisha wote watatu (England, Spain na China) ili kuweza kuondoa hasara kubwa haswa katika matangazo ya television na pia China kufaidika kiuchumi pia katika uhusiano huu.

Ipo Hivii…

Kuna kipindi vilabu vya England na Spain vilikuwa vinaangalia namna ya kuteka soko la Asia na Marekani . Kuliwahi kutoka mpaka wazo la El Classico kuchezwa Marekani . Na kuna wakati baadhi ya mechi za La Liga zilikuwa zinachezwa mchana ili ziendane na muda mzuri kwenye nchi za Asia hasa hasa China.Hii yote ilikuwa ni namna ya kuliteka soko la Asia na Marekani.

Real Madrid vs Liverpool.

Kwanini kipindi hiki wachezaji wa vilabu vya EPL na Laliga wasiwekwe Quarantine kwa muda wa siku kumi na nne pamoja na waamuzi wa EPL na Laliga baada ya siku kumi na nne Ligi ikimalizikie China ambako hakuna maambukizi mapya ya Corona , iwe nafasi nyingine ya kuteka soko la Asia.

Kwa kwenda kucheza  China pia hakika hakuna shaka wala wasiwasi wa miundombinu wala usalama. Kwa maana China ni nchi iliyojidhatiti katika miundombinu yake yote ya reli, anga na barabara kutokana na kuwa na uchumi imara. Lakini pia kwa miaka ya hivi karibuni wamefanya uwekezaji mkubwa katika miundombinu ya mpira wa miguu wakiwa na viwanja vya kutosha na vifaa vyote vinavyohitajika katika soka la kisasa.

 

Sambaza....