Sambaza....

Kwa mara ya kwanza baada ya Miaka kumi, nchi moja imefanikiwa kuingiza timu nne kwenye hatua ya robo fainali ya ligi ya Mabingwa barani Ulaya, baada ya usiku wa kuamkia leo Liverpool kuungana na Manchester United, Tottenham Hotspurs na Manchester City kwa ushindi wa mabao 3-1 ugenini dhidi ya Bayern Munich.

Mara ya mwisho kwa timu nne za kutoka Taifa moja kutinga hatua ya robo fainali ilikuwa mwaka 2009 ambapo Liverpool, Chelsea, Arsenal na Manchester United zilitinga hatua hiyo ikiwa ni kwa mara ya pili mfululizo baada ya kufanya hivyo pia kwa msimu wa 2007-2008.

Mabao mawili ya Sadio Mane na moja la Van Dijk yalitosha kuikatia tiketi Liverpool ambayo msimu jana walicheza fainali dhidi ya Real Madrid ambao kwa msimu huu wameishia kwenye hatua ya 16 bora.

Katika hatua ya robo fainali England wanaongoza kwa kuingiza timu nne, huku mataifa mengine ya Uhispania, Italia, Uholanzi na Ureno wakiingiza timu moja moja, huku mataifa mengine makubwa kama Ufaransa na Ujerumani wakikosa mwakilishi kwenye hatua hiyo.

Droo ya kupanga timu ambazo zitacheza hatua ya robo fainali itafanyika kesho Ijumaa

Timu kutoka ligi kubwa Ulaya zilizofanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ligi ya Mabingwa Ulaya kuanzia msimu wa 1999-2000
Uhispania England Ujerumani Italia Ufaransa Nyinginezo
2018-19 1 4 0 1 0 2
2017-18 3 2 1 2 0 0
2016-17 3 1 2 1 1 0
2015-16 3 1 2 0 1 1
2014-15 3 0 1 1 2 1
2013-14 3 2 2 0 1 0
2012-13 3 0 2* 1 1 1
2011-12 2 1 1 1 1 2
2010-11 2 3 1 1 0 1
2009-10 1 2 1 1 2 1
2008-09 2 4 1 0 0 1
2007-08 1 4 1 1 0 1
2006-07 1 3 1 2 0 1
2005-06 2 1 0 3 1 1
2004-05 0* 2 1 3 1 1
2003-04 2 2 0 1 2 1
2002-03 3 1* 0 3 0 1
2001-02 3 2 2 0 0 1
2000-01 3 3 1 0 0 1
1999-00 3 2 1 1* 0 1

 

Sambaza....