Baada ya sare ya bao 1-1 na kiwango mujarabu dhidi ya Liverpool jana usiku, kocha mkuu wa Arsenal Unai Emery amesema wamekaribia kutwaa ubingwa wa ligi kuu England.
Emery amekitaja kiwango ambacho wamekuwa wakikionesha kama ni uthibitisho wa kuwa bora na kuimarika tofauti na mwanzoni mwa ligi walipoitwa majina mengi.
“Ligi kuu ndio shindano letu la kwanza kulipa kipaumbele kwa sasa, kuna mechi 38, ni muhimu sana unapocheza na Manchester City, Chelsea na Liverpool na kuonesha kiwango kizuri, inatupa muendelezo mzuri,”
“Lakini mechi nyingine ni muhimu kwa sababu unapata alama tatu, Leo (Jana) ilikuwa kipimo kizuri yaani tunachezaje na timu za kariba ya Liverpool, Labda Baada ya kucheza City na Chelsea leo tupo karibu zaidi kufikia kiwango cha timu bora, tunahitaji kiwango hiki kila mchezo, kila mchezo ni muhimu kwetu,” Emery amesema.
Baada ya sare ya Jana ya bao 1-1 Arsenal sasa wapo nafasi ya tano wakiwa alama nne nyuma ya Liverpool mwenye alama 27 kileleni mwa msimamo baada ya michezo 11.