Sambaza....

WAKATI uongozi wa klabu ukiona ‘aibu’ kumfuta kazi kocha Mrundi, Masoud Djuma klabu Simba SC, mashabiki wengi wa klabu hiyo walianzisha nyimbo za na kuliimba jina la kocha msaidizi ALIYEACHWA jijini Dar es Salaam kwa kile kinachosemwa ‘kuisoma Yanga.’ Bahati mbaya zaidi Yanga SC yenyewe ‘haisomeki’ inashinda kila mchezo licha ya kuwa na kikosi kilichobezwa sana kabla ya kuanza msimu.

DJUMA…..
Ameshajitengenezea alama yake kiufundishaji katika soka la Tanzania. Djuma ni kocha wa kisasa kijana ambaye ‘ana usongo’ wa kutengeneza kikosi kinachocheza vizuri mfumo wa 3-5-2. Uongozi unashindwa ama unaogopa kumfuta kazi Djuma kwa sababu unajua kocha huyo wa zamani wa Rayon Sorts atafichua ‘siri ambazo zinawaumbua mno- wana mabadilko.’

Lakini kama ningekuwa katika nafasi ya kufanya maamuzi ningemuondoa Djuma mara tu baada ya timu kuanza kucheza vibaya huku sababu kubwa ikitajwa Mrundi huyo kuwarubuni baadhi ya wachezaji waandamizi ili timu icheze vibaya na kocha mkuu Mbelgiji. Patrick Aussems aonekane hafai na atimuliwe.

Nilishauri hili la kumuondoa Djuma na nikasema pande zote zinazohusika zingenufaika mara baada ya mchezo wao wa ufunguzi dhidi ya Tanzania Prisons 22 Agosti. Kufikia maamuzi na kuyasimamia ni msingi wa utawala bora.

Masoud Djuma

Simba walipaswa kukaa chini na Djuma na kuzungumza naye jinsi ya kuachana kwa maslai ya pande zote lakini matokeo yake wameanzisha tastizo lingine juu ya tatizo lililokuwepo kwa kumuacha Dar kocha Djuma kwa sababu ‘eti’ aifuatilie Yanga.

Baada ya kuangusha alama mbili Nang’wanda, Mtwara na nyingine tatu Kirumba Stadium kikosi cha Aissems hakijafunga goli lolote katika dakika 180 zilizopita na sababu kubwa ni kocha huyo Mbelgiji kushindwa kuipanga timu yake katika usawa.

Kumuacha Djuma Dar huku timu ikitaabika ugenini hakuna faida yoyote kwa sababu hadi mechi na Yanga itakapofika kuna uwezekano wakawa nyuma ya mahasimu wao hao kwa alama tano ama zaidi.

Je, wanaweza kuifunga Mwadui FC katika uwanja wa Kambarage, Shinyanga mwishoni mwa wiki hii? Bila Djuma watachapwa tena lakini wanaweza kuinuka kama watamfukuza kabisa na si kuendelea kumuacha Dar kwa ‘vijisababu’ eti anaifuatilia Yanga!! Huo ni uongo ambao unawaathiri wao wenyewe kama klabu-kama timu.

Nilisema wiki iliyopita, presha kwa Aussems itaanzia Mtwara na uko ndiko tutaanza kujua uwezo wake alisi. Presha imeanza, timu haifungi na mashabiki wake wanaimbia jina la ‘mtu asiyependwa na uongozi-Djuma’ Nini hatma ya Simba baada ya kichapo cha leo vs Mbao FC? KAMA WATAENDELEA KUWA NA Djuma watachapwa na Mwadui, Yanga nao watawapiga na pesa zao. Mfukuzeni Djuma sasa ili Aussems akose sababu.

Sambaza....