Sambaza....

Msemaji wa klabu kongwe nchini Dar Young Africans, Dismas Ten amewaomba radhi watanzania kutokana na kile kilichokuwa kikiwekwa kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram.

Ten ambaye kwa majuma kadhaa sasa amekuwa akiweka taarifa za kuwaponda watani zake Simba SC kwenye ukurasa wake huo, ameonesha uungwana kwa kuwaomba radhi na kutoa ufafanuzi wa kile ambacho kilikuwa kikiendelea kwenye ukurasa wake.

“Naomba radhi kwa post kama 20 ambazo zimekukwaza kwa njia moja au nyingine ,sababu hazikuwa post zenye busara na hekima,” amesema.

Ameendelea kuandika kuwa “Nimepata dhamana kubwa sana na heshima kuwa afisa habari wa club kubwa nchini Tanzania, Young African na sipo tayari kuharibu heshima yangu pamoja na taswira ya club yangu.”

“Kuna mtu ambaye ametumia vibaya account hii,bila kujali heshima,busara na utu wa rika la watu wanaopenda kujifunza na kusikia taarifa muhimu kuhusu club yetu na mambo ya msingi. Kazi yangu inahitaji usafi wa kinywa ,maandishi na weredi , sorry kwa makosa yote yaliyojitokeza..! yatafanyiwa kazi na kuwekwa sawa..!” amefafanua.

Japokuwa ameandika waraka huo lakini baadhi ya wale ambao wanamfuata wameonesha kuingia na shaka kidogo kutokana na sababu alizozianisha “Wewe muongo ni wewe mwenyewe pumbavu Mimi ni mshabiki was yanga,sikupendi wewe Kaka huna faida yoyote kwenye clabu yet ,pambana na maisha yako,” ameandika aminaha749.

Hata hivyo kuna wengine ambao wameonesha kuupokea msamaha huo na sababu ambazo amezioanisha “Hongera kaka wewe ni mmoja wa maafisa habari wa kuigwa no body is perfect,” ameandika chalessjonass.

Ukwel nmekuelewa kuomba msamaha ni jambo la kiungwana lkn kusema haukuwa ww inaondoa maana ya ww kuomba msamaha nadhan ungejikita zaidi kweny kuomba tu msamaha na si kujitetea km umedhamilia kufanya hivyo,” ameandika meena_machibulla

Kwa majuma kadhaa Ten alikuwa akiweka tambo zake ambazo zilikuwa zikisilibwa na mashabiki wake, mashabiki wa Simba na hata wale wa Yanga kutokana na maudhui yaliyokuwa yakiambatanishwa.

Sambaza....