Baada ya kupata nafasi ya kutumbuiza kwenye tunzo za CAF, mwanamuziki nyota wa Tanzania, Diamond Platinumz ameelezea vitu ambavyo amejifunza kwenye tunzo hizo.
“Wakati nipo Cairo kila mtu niliyekuwa nazungumza naye alikuwa anamzungumzia Mbwana Samatta, natamani tungekuwa na watu wengi wanaiowakilisha nchi ” -alisema Diamond.
Alipoulizwa namna alivyojipanga kuandaa vijana ambao watakuwa wachezaji mpira mahiri duniani , amedai anao huo mpango
“Tuko kwenye mazungumzo mazuri na Samuel Etoo, tunapanga mipango mizuri na Samuel Etoo ili kujenga academy , tutashirikiana na wataalamu wa Etoo na watu wa hapa”.
“Kuna wakati nilipokuwa na Samuel Etoo nyumbani kwangu alikuwa anapigiwa simu na watu wa Barcelona waliokuwa wanamtaka Kelvin John. Samuel Etoo alikuja kumwangalia yeye ”
Alipoulizwa kuhusu suala la yeye kumiliki timu ya mpira wa miguu , Diamond Platinumz anadai akipata timu iliyo ligi kuu anainunua.
“Sutaki timu ambayo iko chini ,nataka timu ya ligi kuu ambayo tutakubaliana nayo wabadilishe jina tuiite Wasafi FC , afu naiununua “.
Pia Diamond Platnumz alitoa ushauri kwa vilabu kuwa brand wachezaji wa ndani zaidi kuliko kuwabrand wasemaji wa vilabu.
“Tunatakiwa tuwabrand wachezaji wetu ili wajulikane kuliko wasemaji , mimi nawajua wachezaji wengi wa nje kuliko wachezaji wa ndani.”