Sambaza....

Ni jua la utosini nikiwa nimetulia kwenye viunga vyangu Mbezi Beach. Nikatafakari kidogo na kugundua kuwa wachezaji watukutu wengi ni mafundi wa mpira. Ebu fikiria mtaalamu na mtukutu kama Mido, Joey Burton, Balotelli, Al Hadji Diouf, Rooney, Haruna Moshi, Morrison, hawa ni mfano hai wa tafakari yangu ila wapo wengi zaidi ya hawa.

Macho yangu yamebahatika kushuhudia wachezaji wengi wa aina hii. Paolo Di Canio ni Muitaliano aliyekuwa ananikonga moyo kwa ustadi wake uwanjani. Kwa kifupi ni mjuzi wa soka. Binafsi nilikuwa namuona kama Zidane jinsi alivyokuwa na skills anapokuwa na mpira na mwenye kujiamini.

Paul Di Canio.

Pamoja na ufundi huo, huyu mdau alikuwa ni miongoni mwa wahuni dimbani. Tukio moja kati ya mengi ni pale alipomsukuma refa Paul Alcock na kumwangusha chini kwenye mechi ya ligi kuu kati Shiefield Wednesday na Arsenal mwaka 1998. Kwa tukio hilo alipigwa kadi nyekundu na akafungiwa asicheze mechi nane.

Mimi naamini mtu huwa anatabia zote na uhukumiwa kwa zile zinazotawala zaidi kwenye maisha yake.

Paul di Canio akiudaka mpira badala ya kufunga baada ya mlinda mlango wa Everton Paul Gerald kuumia na kuangika chini.

Mwaka 2001 Di Canio alishinda tuzo ya FIFA ya mchezo wa kiungwana yaani fairplay. Ilikuwa ni kwenye mchezo wa ligi kuu kati ya Everton dhidi ya West Ham Utd disemba 2000. Di Canio akiwa kwenye nafasi ya kufunga aliudaka mpira kama fairplay baada ya kumuona golikipa Paul Gerrard wa Everton kaanguka baada ya kuumia.

Zikiwa zimesalia dakika tano matokeo yakiwa ni 1-1 huku West Ham wakihitaji point tatu muhimu, wana London wengi hawakumuelewa Di Canio akiwepo kocha wake Harry Redknapp.

Sambaza....