Kiungo mshambuliaji wa Dodoma Jiji Fc ni anasubiri muda tu kupaa zake kwenda katika klabu yake mpya ya Al-Hilal ya nchini Sudan baada ya kukamilisha kila kitu kwenye uhamisho wake huo.
Akizungumza na tovuti ya Kandanda.co.tz David Ricard Ulomi amefunguka mengi kuhusu safari yake hiyo kuelekea klabu yake mpya huku ikiwa ni mara yake ya kwanza kwenda kucheza ughaibuni.
“Walianza kunifwatilia muda tuu kumbe hata kabla ya kusaini Dodoma Jiji, waliniona na wakaomba video zangu wakatumiwa mechi nilizocheza na kocha akapendekeza jina langu kusajiliwa katika timu yake.” David Richard
Al Hilal walimuina kupitia michezo ya Ligi Kuu ambayo huonyeshwa na kituo cha Azam Tv. Mara nyingi amekua akicheza kama kiungo wa pembeni kulia au kushoto lakini pia anaweza kucheza nyuma ya mshambuliaji kama namba kumi.
David Ricard mchezaji wa zamani wa Alliance Fc na Ruvu Shooting hakua tayari kuweka wazi maslahi yake mapya katika klabu yake hiyo mpya licha ya kukiri ni mshahara mnono kulingana na Dodoma jiji.
“Mshahara wangu ni mnono sana tu zaidi ya Dodoma Jiji, si vyema kuutaja hapa lakini ni mshashara mzuri sana tu.
Binafsi nimejiandaa vizuri kukabiliana na changamoto, lakini pia nataka kuitumia Al-Hilal kama njia. Al Hilal ni timu kubwa lakini zipo timu kubwa zaidi, kwaiyo ni kupambana juu chini ili niweze kupata timu bora zaidi iwe kama njia kwamimi kufika mbali zaidi.” David Richard