Sambaza....

Kiungo mshambuliaji Joe Cole ambaye amewahi kuhudumu katika timu ya Taifa ya England, na vilabu kama West Ham na Chelsea ametangaza kutandika Daluga baada ya miongo miwili ya kusakata kandanda.

Cole mwenye umri wa miaka 37 amecheza zaidi ya mechi 700 kwenye maisha yake ya soka katika vilabu saba tofauti na amesema baada ya hapo anafikiria kuingia katika tasnia ya ukocha.

Cole amecheza mechi 716 za ushindani na kufanikiwa kufunga mabao 104 katika vilabu saba, huku akiiongoza England katika michezo 56 na kufanikiwa kushiriki fainali tatu za Kombe la Dunia kwenye maisha yake yote ya soka.

“Nahisi kama ndoto imekuwa kweli katika maisha yangu ya soka, chochote kinachokuja baada ya hapa nitakuwa tayari, naamini miongo miwili mingine ijayo itakuwa bora nay a kukumbuka kama iliyopita,” Cole amesema.

“Baada ya miaka 20 kama mchezaji wa mpira naamua sasa kustaafu, muda umefika kwa mimi kutandika Daluga, ni kama ndoto iliyokuwa kweli,,” amesema.

Cole alianza kucheza soka la ushindani akiwa na umri wa miaka 19 akiwa na Hammers na kuonekana kama kipaji kilichokua kwa kasi, na alikuwa miongoni mwa vizazi vilivyoitwa vya dhahabu nchini Uingereza akichipukia na wakali kama David Beckham, Wayne Rooney, Rio Ferdinand, Paul Scholes, Michael Owen na Steven Gerrard.

Klabu yake ya mwisho kuitumika ilikuwa ni Tampa Bay Rowdies inayoshiriki ligi daraja la kwanza nchini Marekani.

Sambaza....