Sambaza....

Jana duniani ya soka imeshuhudia moja ya game ya maana katika hatua ya robo fainali
Kiukweli game hii ilikuwa na hadhi ya fainali yaani ni’ final before final’ pale Santiago Bernabeu Yeste

Kiukweli Kocha wa Chelsea Thomas Tuchel alilalia upande ambao game itachezwa hivyo hakuwa na ugeni tena na machinjio ya Bernabeu

Game strategic ya Tuchel ilikuwa superb kwa asilimia 100 ikiwanzia kwenye uteuzi wa kikosi na majukumu ya mchezaji moja moja aliyopaswa kuyafanya. Alijua fika Madrid wana formation ambayo imekuwa ya kudumu kwao  ya 4-3-3.

Luca Modric akipambana na Kovacic

Huku ikitegemea silaha yake ya viungo wenye tabia zote zinazotakiwa mchezoni, usahihi wa matendo, uwezo wa kusaidia ushambuliaji na kurudi kusaidia safu ya ulinzi ambapo hapa unawataja Luka Modric, Toni Kroos na Casemiro ambaye hajui kucheka hata kidogo yeye ni kazi kazi.

Wao wanajukumu kubwa la kupeleka mashambulizi katika mstari wa mbele unaojengwa na Kareem Benzema na Vinicious Jr Valvede

Master Plan Tuchel alipanga the same formation lakini aliiongezea mbwembwe na kuonekana kama 4-3-1 -2 akimtaka Mason Mount akaye nyuma ya Kai Havert na Timo Werner awatizame kama V shape.



Huku akikusudia sana Mount kuongeza nguvu idara ya kiungo kwa ajili ya kuwin (numerical superiority) na kuondoa dhana ya man to man kati ya viungo wa pande zote mbili yaani Mateo Kovacic ,Ng’olo Kante Loftus Cheek vs Modric Kroos na Casemiro.

Plan hii ndiyo iliyomfanya akapata uongozi wa bao 3-0 hadi dk 10 za mwisho. Ambapo Master tactician Mzoefu Don Carlo alikuwa anasoma nini akifanye ategue mtego huu hadi alivyowaingiza mchezoni Camavinga na Rodrigo katika dakika 20 za mwisho.

Tuchel na vijana wake watalazimika kujilaumu sana sana kutokubadilisha mbinu mara baada ya mabadiliko ya Camavinga ambaye aliongeza kitu kikubwa uwanjani.



Lawama nyingine kwa Tuchel ni kuifanya game mpya kama haina muunganiko na ile ya mwanzo ya Stanford Bridge nani ni hataruli kwao kama ilivyo Vinni Jr na Kareem Benzema.

Nadhani baada ya uongozi wa bao 3-0 aliamini kazi imeisha, Benzema na Vinni jnr hawakupewa ulinzi unaostahili.
Kama Tuchel na jeshi lake wangejua na kuamini uhatari wa wawili hao huwenda matokeo yasinge kuwa haya. 

Mwisho wa Yote baada ya matokeo haya nawaona Real Madrid kwenye kibarua kizito tena kati ya City au ATM.

Sambaza....