Sambaza....

Kocha Msaidizi wa Wanalambalamba Azam FC, Nassor Idd Cheche anatarajiwa kuongoza Msafara wa wachezaji wa Azam kuelekea nchini Zimbabwe katika mechi yao ya Marudio dhidi ya Triangle katika michuano ya Shirikisho Afrika.

Azam wanatarajiwa kuondoka katika mafungu matatu. Fungu la kwanza litaondoka siku ya Jumapili ya tarehe 22. kundi hili litakuwa na wachezaji ambao hawajaitwa katika timu ya taifa inayojiandaa na mchezo dhidi ya Sudan katika michuano ya kufuzu Chan.

Kundi hili litaongozwa na kocha Msaidizi Idd Cheche, kabla ya tarehe 23 ambapo kundi la pili la wachezaji pamoja na kocha mkuu Ettiene Ndayiragije ambaye ndiye kocha wa Taifa Stars kuungana na wenzao nchini Zimbabwe.

Kundi hili litahusisha kocha na wachezaji watano wa kikosi hicho ambao walikuwa na mwalimu katika majukumu ya kitaifa. Wachezaji hawa ni Idd Selemani, Frank Domayo, Mudathir Yahya, Shaaban Idd na Salum Aboubakar.

Kundi la tatu linatarajiwa kuungana na timu siku chache kabla ya mechi. kundi hili litahusisha viongozi wa timu, lengo ni kuungana na wachezaji na benchi la ufundi kuwatia moyo zaidi na kuhakikisha wanapata matokeo chanya.

Azam wanatarajiwa kuwavaa Triangle Septemba 28. Katika mchezo huu Azam inatafuta ushindi wa aina yoyote ile, kwa maana kama watapata ushindi mwembamba wa goli 1-0 watapata nafasi nyingine katika mikwaju ya penati, ushindi mwingine zaidi ya hapo kutaifanya Azam isonge mbele.

Mtandao huu unajua kuwa Azam ina kikosi kizuri, licha ya kupoteza nyumbani kwa goli 1-0, Azam wanaweza fanya vizuri katika mchezo wa ugenini.

Mungu Ibariki Tanzania, Mungu ibariki Azam

Sambaza....