Sambaza....

Ligi ya Championship zamani Ligi daraja la kwanza imeendelea kushika kasi katika viwanja mbalimbali nchini huku ikielekea ukingoni na kupeleka kuongeza ushindani.

Leo Jumamosi timu 14 zimeshuka dimbani kwa maana michezo 7 ya Ligi hiyo imepigwa huku Jkt Tanzania akionekana kuzidi kuweka mazingira mazuri yakurudi Ligi Kuu kwa kuzidi kujichimbia kileleni.

Jkt Tanzania wakiwa nyumbani kwao uwanja wa Meja Jenerali Isamihyo wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao moja bila mbele ya maafande wenzao Transit Camp. Ushindi huo unawafanya kufikisha alama 56 kileleni.

Kitayosce nae akiwa nyumbani amefanikiwa kupata ushindi wa mabao matatu kwa mawili mbele ya Biashara United na kufikisha alama 49 na kuendelea kujikita nafasi ya pili wakati Pamba wao wamepata ushindi wa mabao mawili kwa moja ugenini dhidi ya Green Worriers na kufikisha alama 47 wakishika nafasi ya tatu. 

Matokeo mengine katika Ligi hiyo ya michezo ya leo ni, Fountaine Gate wametoka suluhu na Pan Afrika kama ambavyo mchezo kati ya African Sports na Ken Gold ulivyomalizika. Mashujaa wamepata ushindi wa bao dhidi ya Copco na Mbuni wameifunga Mbeya Kwanza mabao mawili kwa moja.

Ligi hiyo imeendelea kushika kasi huku timu za JKT Tanzania, Pamba Fc, Kitayosce na Mashujaa zikipambana kupata nafasi ya kupanda Ligi kuu wakati chini ya msimamo pia kuna Ndanda, Transit Camp, Green Worries, Copco na Pan Afrika zinapambana zisishuke daraja. 

 


Sambaza....