Sambaza....

Kiungo fundi Mzambia Cleotas Chota Chama anaekipiga katika klabu ya “Wekundu wa Msimbazi” Simba sc ameendelea kufanya vibaya katika michuano ya Kimataifa baada ya juzi Simba sc kufungwa ugenini mabao mawili kwa sifuri na JS Saoura nchini Algeria.

Mpaka sasa amecheza mechi zote za Ligi ya Mabingwa akiwa na klabu yake ya Simba sc huku akiweza kufunga jumla ta mabao manne tangu hatua za awali mpaka hatua za makundi.

Chama amekua akicheza vizuri katika uwanja wa Taifa “Kwa Mkapa” jijini Dar es Salaam akiwa na Simba lakini hali huwa tofauti anapokua katika viwanja vya ugenini, Chama huwa anapoa na kupotea kabisa katika michezo ambayo Simba anacheza ugenini.

Katika michezo yote ambayo Simba imecheza ugenini katika kundi D imepata kichapo na michezo yote Chama huanza katika kikosi cha kwanza. Alianza kwenye mchezo dhidi ya AS Vita Simba ikapigwa 5 halafu ukaja mchezo dhidi ya Al-Ahly tena Simba ikapigwa tano na mchezo wa mwisho ni dhidi ya JS Saoura Simba ikapoteza kwa mabao mawili.

Katika michezo yote hiyo Chama amekua akionyesha kiwango duni na kushindwa kabisa kuonyesha makeke yake na hivyo kupelekewa kutolewa uwanjani.
Kwa uwezo alionao Cleotus Chama haswa anaouonyesha katika Ligi yetu ni wazi alitegemewa acheze pia katika kiwango cha juu na kuisaidia Simba katika Ligi ya Mabingwa kutokana uzoefu wake pia lakini imekua kinyume. Chama ameshindwa kabisa kuisaidia Simba katika michezo ya Kundi D ya Klabu Bingwa Africa.

Je Cleotus Chama ni wakutesa hapa hapaa tuu katika Ligi yetu? Je ataedelea kutesa kwa vilabu vyetu vya ndani tuu lakini sio na vilabu vikubwa Africa katika Ligi ya Mabingwa?

Sambaza....