Sambaza....

Timu ya Stand United “Chama la wana” ya Shinyanga imekuwa timu ya kwanza kuingia nusu fainali ya Azam Sports Federation Cup (ASFC), baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Njombe mji FC ya Njombe

Mchezo huo uliopigwa kunako uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga, Stand United ilijipatia bao hilo la pekee kupitia kwa Bigirimana Bleise dakika ya 12, akimalizia kazi nzuri ya Vitalis Mayanga

Dakika ya 80, Stand United ilipata pigo baada ya nahodha wake Erick Mulilo kutolewa nje kwa kadi nyekundu kufuatia kuoneshwa kadi ya pili ya njano

Baada ya ushindi huo, Stand United sasa itakutana na mshindi wa mchezo kati Azam FC na Mtibwa sugar, katika nusu fainali inayotaraji kupigwa kati ya Aprili 16 na 18

Robo fainali zingine za michuano hiyo, inataraji kuendelea tena kesho ambapo Tanzania Prisons itaikaribisha JKT Tanzania mchezo utakaopigwa kunako dimba la Sokoine majira ya saa 10:00 jioni

Azam FC, watakuwa mwenyeji wa Mtibwa sugar kunako uwanja Azam Complex uliopo Chamazi mchezo utakaoanza majira ya saa 2:00 za usiku

Hatua hiyo ya robo fainali ya Azam Sports Federation Cup, itakamilika Jumapili ambapo Singida United watakuwa nyumbani kuwakaribisha Yanga sc kunako uwanja wa Namfua mjini Singida

Sambaza....