Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limetangaza tarehe rasmi za mechi za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2023. Kombe la Mataifa ya Afrika 2023 litashiriki Ivory Coast kwa mara ya kwanza tangu 1984, wakati Cameroon ilipoifunga Nigeria katika fainali.
CAF ilionyesha katika toleo la 34 la mashindano ya AFCON litafanyika kuanzia Jumamosi, 13 Januari 2024, hadi 11 Februari 2024. Na mpaka sasa tayari kuna mataifa saba ambayo yamejihakikishia nafasi ya kushiriki mashindano hayo, ambayo ni wenyeji Ivory Coast, Algeria, Morocco, Afrika Kusini, Burkina Faso, Tunisia, na mabingwa wa Afrika Senegal.
Tanzania inahitaji ushindi katika michezo miwili iliyosalia dhidi ya Niger nyumbani na Algeria ugenini huku pia wakiomba matokeo mabaya kwa Uganda ili kuungana na Algeria ambao wameshafuzu katika Kundi F.
Kwa Tanzania sasa inatafuta kufuzu kwa mara ya tatu na mara ya mwisho kushiriki michuano hiyo ilikua ni mwaka 2019 ambapo tuliaga mashindano katika hatua ya makundi mbele ya Senegal na Algeria walioibuka vinara na kusonga mbele ambao pia walitinga fainali.