Sambaza....

Jumla ya wachezaji 20 wa kikosi cha timu ya soka ya Simba SC pamoja na baadhi ya viongozi wanatarajia kuondoka kesho jioni tarehe 29, 01, 2019 kwa ajili ya mchezo wa tatu wa hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya Mabingwa Afrika, dhidi ya timu ya soka ya Al Ahly.

Taarifa ya klabu kwa vyombo vya habari imesema Simba itaondoka na ndege ya Shirika la Ethiopia, kupitia Addis Ababa nchini Ethiopia na kasha kuelekea mjini Alexandria ambapo ndipo watakapocheza na Al Ahly siku ya Jumamosi ya Februari 2, 2019.

Katika msimamo wa kundi D Simba inashika nafasi ya tatu baada ya kucheza michezo miwili, wakishinda mchezo mmoja dhidi ya Jeunesse Sportive de la Saoura kwa mabao 3-0 jijini Dar es Salaam kabla ya kwenda kupokea kichapo kikali cha mabao 5-0 kutoka kwa AS Vita ya nchini DR Congo, wakati wenzao Al Ahly ambao wanaongoza kwa alama nne hawajapoteza mchezo wowote kwenye hatua ya makundi wakishinda 2-0 dhidi ya AS Vita na wakitoka sare ya 1-1 dhidi ya JS Saoura.

Wakati huohuo klabu ya Simba imemtangaza Patrick Rweymamu kuwa meneja wa muda kikosi hicho kuchukua nafasi ya Abbas Ally ambaye naye alikaimu nafasi hiyo kwa muda sasa toka Kamati ya maadili yaShirikisho la soka nchini ilipomfungia  mwaka mmoja Robert Richard kutokana na kuihujumu timu ya Taifa.

Sambaza....