Sambaza....

Wanangu mliovaa majoho kitambo nawasalimu kwa heshima kubwa bila kusahau wenzangu wenye ujuzi mkubwa lakini mitaa bado haijatuelewa, tujipige kifuani huku tukisema Kila Jambo na Wakati Wake, (Amen)

Ulishawahi kuzunguka na CV/Vyeti zako kwenye ofisi mbalimbali mpaka CV yenyewe ikachakaa? Hahaahah nacheka lakini inauma kinoma, wahanga mnanielewa naamini, inafika muda unaitafuta bahasha ya kaki kwambinde na hauipati Daah!! (inshaalah)

Basi hii ni taswira kamili ya mwanasoka Bruno Miguel Borgers Fernandes mzaliwa wa Maia pale Ureno, kwa Mashabiki wa timu ya Manchester United kule Uingereza.

Haukuwa mwanzo mzuri kwa Mashetani hao Wekundu kwenye ‘EPL’ msimu wa 2019/20, mpaka pale February Fernandes alipovaa jezi ya Mashetani hao Wekundu yenye namba 18 mgongoni dhidi ya Wolves.

Baada ya Sosha ‘Ole Gunnar’ na mashabiki wa MUFC, kuzunguka na barua za kutafuta ushindi bila mafanikio kwa muda mrefu, gafla bahasha ikapatikana ya kuziweka barua zile, ndio ni Bruno Fernandes. Kazichukua barua zote kazitia ndani ya bahasha yake, barua zile za ‘Sosha Out’, ‘Pogba out’ sijui nini na nini, yaani zoote kazitia kwenye bahasha moja na zimetulia.

Paul Pogba na Bruno Fernandes!

Leo hii husikii nyenyenyee wala nyinyinyii, mashabiki wa MUFC wametulia tuliii wanajinenepea. Toka avae uzi ule wa MUFC, dimba limechangamka, mbungi inapigwa na wanatoboa, kandanda inatandazwa, nini kingine United mnataka?

Kuna muda nawaza kwanini Bruno alikua kule Ureno muda wote ule, mtu wa mpira vile, kiungo mchakalikaji, akili kibao kwa kichwa fundi anayeipa hamasa timu, kisha nakumbuka kuwa hata wana wa Israel walisota saana mpaka pale alipotokea Musa na kuonesha njia.

Anthony Martial akishangilia na Bruno Fernandes.

Mkishampa Rashford huo u’daktari wa heshima, basi Mpeni na Bruno Uganga wa heshima😂.

Sambaza....