
Mshambuliaji wa Liverpool na timu ya taifa ya Misri, Mohamed Salah ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa mwaka 2018.
Katika kinyang’anyiro hicho Salah amempiku rafiki yake Sadio Mane ( Liverpool) na Pierre Aubameyang wa Arsenal.
Tuzo hiyo, inamfanya Salah achukue mara ya pili mfululizo.