Inawezekana kuna swali kubwa ambalo huwa linazunguka kichwani mwako, ni kipi kilikuwa chanzo kikuu cha Rais wa awamu ya tatu Ndg Benjamini William Mkapa kujenga kiwanja cha taifa.
Mwaka 2003 baada ya Simba Sponga kuiondosha Zamalek kwenye Michuano ya Vilabu Bingwa vya Afrika.
Siku hiyo hiyo Bwana Benjamin William Mkapa Rais wa Awamu ya Tatu alikuwa anarudi Nchini kutoka ziara yake ya Nje ya Nchi!
Akashangazwa sana na Hali aliyoikuta pale Uwanja wa Ndege wa Julius Kambarage Nyerere
Watu walikuwa Wengi kweli kweli
Watu walikuwa wengi wasiojesabika
Mawazoni mwake alihisi watu wale wamekuja kumpokea yeye
Lakini akashangaa hawakuwa na Time nae hata kidogo wala kujua kama Rais alikuwa ametua kwenye Uwanja wa Ndege wa JKNIA muda huo
Ndipo akauliza Hawa watu wanafanya nini hapa? Mmoja wa Wasaidizi wa Rais wakati huo akamwambia Hao ni Washabiki wa Simba Sponga Timu Bora kuliko zote kupata kutokea kwenye Umbwe la Ardhi ya Nchi hii!
Rais akawa na Shauku zaidi kutaka kujua sasa kwanini wapo Airport washabiki wa Simba Sponga?
Akaambiwa Usiku wa Jana Simba Sponga waliibutua Zamalek huko kwao Cairo Misri na Kutinga Nane Bora za Afrika kwenye hatua ya Makundi!
Ndipo hapo Anko Benja akabaki mdomo wazi na Kusema Watu wa Nchi hii wanapenda Mpira na hivyo Basi kabla sijaondoka Nitawaachia Zawadi ya Kiwanja Kikubwa zaidi ya Cha Sasa!
Ndipo Kikashushwa kiwanja kile cha Benja pale Temeke pembeni kidogo ya Uwanja wa Uhuru sasa ambao before ulijulikana kama Uwanja wa Taifa!
Credit kwa Mdidi the Writer ‘19