Shangwe, vifijo na nderemo jana vilitawara katika mkoa wa Mara, baada ya timu yao ya soka ya Biashara kufanikiwa kupanda ligi kuu ya soka Tanzania bara
Biashara imefanikiwa kupanda baada ya kuitandika Transit camp kwa mabao 3-2 katika mchezo uliokuwa mkali na wa kusimua kwa dakika zote 90
Kwa matokeo hayo yanaifanya Biashara kuongoza kundi C kwa kufikisha jumla ya alama 30, huku ikuatiwa na timu ya Alliance yenye alama 28
Katika mchezo mwingine uliopigwa kwenye uwanja wa Nyamagana mjini Mwanza, timu ya Alliance imefanikiwa kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Jkt Oljoro
Ushindi huo umeifanya Alliance kumaliza ikiwa nafasi ya pili kunako kundi C nyuma ya Biashara, hivyo kuungana pamoja kupanda ligi kuu msimu wa 2018/19
Biashara na Alliance zinakamilisha idadi ya timu tano zilizokata tiketi hiyo, ambapo timu zingine ni Coastal Union ya Tanga, Jkt Tanzania, KMC ya Dar es salaam
Nafasi moja imesalia ili kukamilisha idadi ya timu sita, zinazotakiwa kupanda msimu ujao wa ligi kuu