Hali si shwari ndani ya klabu ya Simba haswa katika eneo la benchi la ufundi huku kila kukicha zinaibuka tetesi mpya za kuvunjwa kwa klabu ya Simba huku wengine wakihusishwa na kupata kibarua kwingineko.
Achana na tetesi za kocha mkuu Sven Vandebroeck kukatwa mwisho wa msimu na nafasi yake akitajwa kuchuliwa na Florentine Ibenge, ishu ni stori mpya ya kocha msaidizi pamoja na meneja wa timu.
Iko hivi Azam fc wanataka kuwang’oa kocha msaidizi wa Simba Selemani Matola pamoja na meneja wa muda mrefu Simba Patrick Rweyemamu. Wawili hao wanatajwa kuelekea Azam fc msimu ujao kuanza maisha mapya chini ya tajiri Yusuph Bakresa.
Wawili hao watakumbukwa kwa uwezo wao mkubwa wa kuandaa vijana wadogo katika misingi ya soka na kuipa faida Simba sc na Taifa kwa ujumla. Miongoni mwa nyota walipotia mikononi mwao ni pamoja na Said Ndemla, Ibrahim Ajib na Miraj Athuman ambao wapo Simba mpaka sasa. Lakini pia kina Hassan Hateeb, Abdallah Seseme, Raymond Dotto, Japhet Makarai ni miongoni mwa nyota wa VPL waliopita mikononi kwa Matola kama kocha huku Rweyemamu akiwa meneja.