Klabu ya soka ya Barcelona ya nchini Hisapania imetema cheche katika usajili wa dirisha dogo majira ya baada ya kuanza kutumia fedha zake kwa kumchukua mshambuliaji Mghana kutoka Seria A.
Barcelona imemsajili Kelvin Prince Boateng kwa mkopo wa miezi sita huku wakiwa na uamuzi wa kumnunua jumla ifikapo mwisho wa msimu. Kevin Prince alikua akiichezea klabu ya Sassuolo ya nchini Italia inayoshiriki Seria A.
Barcelona wamelipia €2 millioni huku wakitegemea kulipia €8.2 mwisho wa msimu ili kumsajili jumla Mghana huyo ndugu yake Jerome Boateng anaekipiga Bayern Munich. Wa kumsajili Boateng Barcelona inakua imeongeza nguvu katika safu yake ya ushambuliaji ili kuendelea kiwania taji La Liga.
Mashabiki wengi wa soka wamekua wakibeza usajili huo huku wakisema Barca wameishiwa. Laikini Boateng ni mzoefu wa ligi ya La Liga, ikumbukwe alikuepo katika ligi hiyo akiwa na wabishi wa Las Palmas msimu wa mwaka 2016/2017.