Limekuwa kama ajabu la 8 la dunia kwa Barcelona kutolewa katika hatua ya robo fainali ya Europa league. Ajabu kivipi? Barca wanasifa kubwa ya kubadili matokeo wakiwa kwenye uwanja wao wa nyumbani Camp Nou
Tangu zama na zama lakini kwa matokeo aliyoyapata Entrach Frankfurt 3-2 inaonesha napo pameanza kuwa kama ‘shamba la Bibi’.
Hakuna aliyetarajia kuona Frankfurt wakitoka na ushindi mnono wa 3-2 na muda mwingi wa mchezo wageni walikuwa wanaongoza 3-0 ambayo mimi hupenda kusema (3 -nyau).
Baada ya kutolewa kwenye league ya mabingwa mahujaji walikuwa na hoja ya kwamba Barca anakwenda kutwaa kombe la Europa league kwa kuwa wanakikosi kizuri ambacho kilikuwa na sifa hata ya kutwaa ubingwa wa UEFA champion league.
Barcelona wamekuwa akiajiri makocha siku za karibuni kwa kuangalia DNA, je Kocha alipita kwenye club au alicheza? Wachukue hawa wawili waliopishana Ronald Koeman na huyu wa sasa Xavi Harnandez achana na Mzee wetu Quique Satien.
Ukimuangalia Xavi pamoja na kusajili wachezaji kama 4 wa dirisha dogo akiwemo rafiki yake Dan Alves, Aubameyang Torres na Adama Troure na kutokupata muda wakutosha kuimplement filosofia yake lakini mashaka ni sehemu ambayo ameenda kupatia uzoefu Qatar.
Barcelona ya Xavi ndiyo kwanza jahazi linakwenda ‘mchomo’ zaidi hata kwenye michuano miyepesi ambayo intensity yake si kubwa kuliko Champion League ameshindwa kufanya vizuri.
Nadhani kuna haja ya kuachana na dhana ya kutumia wachezaji waliopita katika club wakati wa Career zao wakiwa wachezaji kabla ya kuturn kwenye Coaching.
Hapa ndiyo utakubaliana nami zimwi likujualo halikuli likakwisha ‘ lazima Joan laporta na jopo lake la maamuzi wafikie hatua kuachana na dhana hiyo.
Binafsi namuona Xavi licha ya kucheza kwa mafanikio bado kuchukua timu kubwa kama hiyo na kuisogeza mbele. Naona kama timu itazidi kudidimia na mwisho wa siku itapotea kwenye ramani ya ushindani wa Ulaya.
Na hata ndani ya La liga mwendo si mzuri ubingwa kama tayari kuna 75% ya kuelekea kwa mahasimu wao Real Madrid na hivyo kufanya kupokezana katika jiji hilo maana bingwa mtetezi ni Atletico Madrid na kuendelea kuwaweka pending kwa miaka kadhaa.