- Safari ya Yanga, Mikononi mwa Dube
- Simba na Yanga nani anaongoza kuweka mpira kwapani.
- Yanga Waweweseka! Gamondi Nje!
- Fadlu Tunaamini anawapa Ubingwa Wekundu
- Manuel Neuer ana umri sawa na uchambuzi wa soka kwa kompyuta
Mwanzoni mwa msimu kulikuwa na mjadala mkubwa sana kuhusiana na upana wa kikosi cha Simba. Mjadala ambao kwa kiasi kikubwa ulianzishwa na Haji Manara.
Msemaji wa Simba, msemaji anayeisemea Simba kwa moyo wote. Msemaji anayeipenda Simba kuliko hata chakula chake cha mchana.
Pumzi anayoivuta ina rangi nyekundu na nyeupe. Kwa kifupi Simba ipo karibu kabisa na moyo wake, ni hatua chache sana ambazo zinatenganisha mapenzi ya manara kwa Simba pamoja na moyo wake.
Ni vitu viwili ambavyo viko karibu sana na ni majirani wazuri sana. Ndiyo maana maisha ya Haji Manara yametawaliwa na Simba.
Kuna wakati Simba ukiitaja lazima jina la Haji Manara lije kichwani mwako, na unapotaja jina Haji Manara, lazima jina la Simba lije kichwani.
Kwa kifupi huwezi kuitenganisha Simba na Haji Manara. Ndiyo maana Haji Manara huona fahari kusema vizuri Simba.
Haijalishi utachukuliaje, haijalishi utakasirika lakini yeye kazi yake ni hiyo tu na anajivunia sana hiyo kazi yake.
Ndiyo maana alitumia muda mwingi sana kuisifu Simba, alitumia muda mwingi sana kuwaambia watu kuwa Simba ina kikosi kipana.
Alitumia muda mwingi kuwaambia wapinzani wake kuwa Simba ina uwezo wa kucheza mechi mbili ndani ya siku moja.
Alilisema hili bila yoga kabisa. Wengi walimshangaa sana. Lakini yeye hakutetereka aliendelea kusimamia alichokuwa anakiamini.
Kiukweli ukiitazama Simba inaogofya sana. Kila idara kuna wachezaji ambao wanakaribiana kiuwezo ndani ya uwanja.
Na hii ndiyo tafasri ya moja kwa moja ya kikosi kipana. Kikosi kipana siyo kuwa na wachezaji wengi tu. Lakini kikosi kipana tafasri yake ni kuwa na wachezaji ambao hawapishani sana viwango.
Ndiyo maana wakati Shomari Kapombe anaumia, Gyan aliweza kutusahaulisha na hata alipokuja Zana Coulibay tukawa tumejisahaulisha kwa muda kuhusu Shomari Kapombe.
Siku Mohammed Hussein “Zimbwe Jr” akiumia kuna Asante Kwasi ambaye hapishani sana kiwango na Zimbwe Jr
Ushawahi kutazama nafasi ya mabeki wa kati, ambapo kuna kina Paul Bukaba, Erasto Nyoni, Pascal Wawa, Juurko.
Safu ya kiungo je ? Safu ya ushambuliaji?. Yani kwa kifupi Simba ina wachezaji ambao wanakaribiana viwango. Na hii ndiyo maana halisi ya kikosi kipana.
Wakati Simba inaenda kucheza na African Lyon kule Arusha ilikuwa imetoka kucheza mechi ya kimataifa, ilifanya mabadiliko kwenye kikosi chake.
Kina Haruna Niyonzima, Hassan Dilunga, Deo Munish, Bukaba, Adam Salamba. Walipata nafasi kwenye mechi hii na Simba ikafanikiwa kushinda 3-0.
Wakati inaenda Iringa kwenye uwanja wa Samora kucheza na Lipuli walikuwa wametoka kucheza na Al Ahly. Kuna wachezaji walipumzishwa na timu ikapata ushindi.
Jana Simba ilikuwa inacheza na timu ambayo inaonekanaga ngumu sana kila inapokutana na vigogo, yani Mbao FC.
Kulikuwa na wachezaji nyota ambao hawàkuwepo kwenye kikosi. Chama, Emmanuel Okwi na Aishi Manula hawakuwepo kwenye mechi hii.
Na ni wachezaji ambao ni muhimu sana ndani ya kikosi cha Simba , lakini wakaingizwa wachezaji watatu kuziba nafasi zao.
Deo Munish “Dida”, Mohammed Hussein na Haruna Niyonzima. Lakini mwisho wa matokeo Simba ikaibuka na ushindi wa 3-0.
Hii ndiyo maana halisi ya kikosi kipana. Kila mchezaji anayeingia kwenye kikosi , timu inakuwa na nafasi kubwa sana ya kupata matokeo ambayo ni chanya.