Nyota wa Klabu ya Yanga kiungo mshambuliaji Stephane Aziz Ki ameibuka kinara katika tuzo za mwezi April baada ya kuchaguliwa kuwa mchezaji bora akiungana na kocha wa Tanzania Prisons Abdallah Mohamed.
Aziz Ki katika mwezi April amecheza michezo miwili dhidi ya Kagera Sugar na dhidi ya Simba, kstika mchezo dhdi ya Kagera Sugar akifunga mabao matatu na kuisaidia Yanga kuvuna alama tatu wakiwa nyumbani.
Nyota huyo kutoka Burkina Faso aliingia fainali dhidi ya Jean Baleke wa Simba na Ayoub Lyanga wa Azam Fc na kufanikiwa kuwapiku na kunyakua tuzo hiyo.
Kwa upande wa makocha Abdalla Bares yeye ameibuka kinara baada ya kubeba alama zote sita katika michezo miwili na hivyo kuwapiku Robert Oliveira wa Simba na Daniel Cadena wa Azam Fc.
Kwa upande wa meneja bora wa uwanja tuzo hiyo sasa ni kama haina mpinzani kwani meneja wa uwanja wa Highland Estate unautumiwa na Ihefu Omar Malule ametwaa tuzo hiyo baada yakufanya hivyo mara nne mfululizo sasa.