Kwa mara ya kwanza klabu ya soka ya JKT Tanzania imepoteza mchezo katika uwanja wake wa nyumbani wa General Isamuhyo Mbweni JKT Dar es salaam katika mchezo dhidi ya AzamFc.
Ikicheza mbele ya mashabiki wake klabu ya Jkt Tanzania imekubali kupoteza mchezo huo na hivyo kua mchezo wake wa kwanza kupoteza katika msimu huu wa Ligi kuu Bara msimu huu.
Ikumbukwe JKT Tanzania wamecheza michezo saba katika dimba hilo bila kupoteza hata mchezo mmoja.
Alikua ni Yahya Zaid alieiandikia bao Azam fc baada ya kazi nzuri ya Donald Ngoma ya kuwatoka mabeki na kumimina krosi murua iliyomkuta mfungaji na kumuacha kipa wa JKT Abdulrahmani akikosa la kufanya. Na hivyo kulifanya bao pekee lililoamua matokeo ya mchezo wa leo.
Katika mchezo huo Azam fc ilibidi kucheza pungufu kwa dakika 50 za mchezo baada ya mshambuliaji wake Mghana Enock Atta Agyei kuonyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja katika kipindi cha kwanza baada ya kumchezea vibaya beki wa JKT Tanzania.
Timu zote mbili zilifanya mabadiliko kwa wakati tofauti ili kuweza kusaidia timu zao kupata matokeo. Kwa upande wa JKT Tanzania walifanya mabadiliko Mara mbili wakiwatoa Kelvin Nashon na kuingia Nasorro kapama, Ramadhani Madenge alitoka na kumpisha
Kwa upande wa Azam waliwatoa Donald Ngoma na Yahya Zayd na nafasi zao kuchukuliwa na Dany Lyanga na Hassan Mwasapili. Pia Tafwadza Kutinyu alichukua nafasi ya Mudathiri Yahya.
Vijana wa JKT Tanzania itabidii wajilaumu wenyewe kwa kukosa angalau alama moja baada ya kupoteza nafasi kadhaa za kufunga kutokana na washambuliaji wake Abdulrahmani Mussa na Hassan Materema kukosa umakini.