Klabu ya Azam fc imefanikiwa kutetea ubingwa wake wa kombe la mapinduzi, baada ya kuilaza URA kwa penati 4-3 kufuatia matokeo ya sare ya 0-0 katika dakika 90 za kawaida
Katika mchezo huo ulioamuliwa na mwamuzi Mfaume Nassor aliyesaidiwa na Mbaraka Haule na Dalila Jaffary, ukihudhuliwa na Rais wa Zanzibar na mwanyekiti wa baraza la mapinduzi Dk Ally Mohammed Shein, ambapo golikipa wa Azam fc Mghana Razack Abalora alicheza penati mbili za Brian Majwega na Patrick Mbowa
Waliofunga penati kwa upande wa Azam fc ni nahodha Himid Mao, Enock Atta Agyei, Yakubu Mohammed na Aggrey Morris huku ile ya Bruce Kangwa ikidakwa na kipa wa URA Alionzi Nafia, penati za URA zilifungwa na Jimmy Kulaba, Charles Sempa na Shafiq Kagimu
Azam fc sasa inakuwa imelitwa kombe la mapinduzi kwa mara ya nne, ikitangulia kufanya hivyo miaka ya 2012, 2013 na 2017
Azam fc iliwakilishwa na Razack Abalora, Himid Mao, Bruce Kangwa, Aggrey Morris, Yakubu Mohammed, Abdallah Kheri/ Joseph Mahundi dk 56 Stephane Kingue, Frank Domayo “Chumvi”/ Iddi Kipagwile dk 55 Salmin Hoza, Bernard Arthur/ Shaban Iddi Chilunda dk 58 na Yahaya Zayed/ Enock Atta Agyei dk 65
URA; Alionzi Nafia, Enock Kibumba, Brian Majwega, Alain Munaba, Patrick Mbowa, Nicholas Kagaba, Julius Mutyaba, Kalama Debos/ Charles Sempa dk 64 Mosses Seruyinde/ Peter Lwasa dk 79 Hudu Mulikyi na Shafiq Kagimu/ Jimmy Kulaba dk 80