Sambaza....

Klabu ya soka ya Azam FC imeendelea kupunguza wachezaji wake baada ya kukosa nafasi ya kucheza mara kwa mara katika kikosi cha kwanza, haswa katika eneo lá ushambuliaji.

Mwalimu Hans Plujim ameamua kuwatoa wachezaji wake wawili wa eneo la ushambuliaji kwa mkopo kwenda kwenye vilabu vingine vya Ligi Kuu Bara ili wapate nafasi za kucheza.

Washambuliaji Ditram Nchimbi na Waziri Junior wametolewa kwa mkopo baada ya kukosa nafasi kutokana na uwepo wa washambuliaji wengine wenye uwezo mkubwa kuliko wao kama Yahya Zaid, Donald Ngoma na Danny Lyanga.

Waziri Júnior amepelekwa kwa mkopo Biashaara utd ya Mara mpaka mwisho wa msimu. Ikumbukwe Waziri Júnior alijiunga na AzamFc akitokea Totó African baada ya kushuka daraja.

Ditram Nchimbi amejiunga na Mwadui FC ya Shinyanga ambapo atakaa huko mpaka mwisho wa msimu. Ditram Nchimbi alisajiliwa na Azam fc akitokea Njombe Mji iliyoshuka daraja.

Sambaza....