Huu si tena wakati wa Aussems kushangilia goli la muijiza ya Chama, ili asiwe jamvi la wageni katika hatua ya makundi afanye jitihada kama kocha kupandisha viwango vya Jjuuko na Kwassi kama anaona hawajakidhi mahitaji yake. Hao ni wachezaji muhimu mno katika ngome yake akiamua wawe.
Wawakilishi pekee wa Tanzania waliosalia katika michuano ya Caf, Simba SC jioni ya Leo watatupa karata yao ya mwisho ili kujaribu kupindua matokeo ya 1-2 vs Nkana Red Devils FC na kufuzu kwa hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa Afrika 2018/19.
Usajili wake wala haukuwashtua wengi, haitoshi, mchezo wake wa kwanza akiwa na jezi za Yanga SC alijifunga na kusababisha penati Agosti, 2017.
Kuelekea mchezo wao wa marejeano wa Caf Confederation Cup dhidi ya KCCA FC ya Uganda kesho Jumamosi, nahodha wa Mtibwa Sugar FC, Shaaban Nditti amekiri watalazimika kucheza ‘kufa na kupona’ ili kupindua matokeo ya 3-0 na kufuzu kwa hatua ya mwisho kuwania nafasi ya kufuzu kwa hatua ya makundi.
Licha ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Mwadui FC kuhitimisha michezo kumi mfululizo bila ushindi katika ligi kuu Tanzania Bara kocha mkuu wa Mbao FC, Amri Said ‘Stam’ amesema hawezi kukubali ujio wa kocha Ally Bushiri.
Kwanini pia Nyika alisema Ilanfya alihitaji Tsh. 25 wakati ukweli mchezaji huyo alihitaji milioni kumi tu?
Beki ya Simba bado ni uchochoro, na wala usiwaze kuhusu 1-0 Dar es Salaam, Nkana watakuja hapo na kufunga tena na si ajabu ni wao wakapita kwa goli la ugenini kwa beki hii ya Simba na golikipa ‘asiyeona kiki za mbali.’
Licha ya udhamini walionao bado Mbao FC ipo katika hali ngumu pia.
Kuwa na Boban, Mrisho Ngassa, Kelvin Yondan,Thaban Kamusoko, Amis Tambwe, Deus Kasekeni faida kubwa kwa Zahera. Kazi kwake.
Je Simba kuvunja huu mwiko? Na Upi utabiri wako pia kuelekea mchezo huu? Mbolembole ameshatoa wake.