Baada ya aliyekuwa kocha mkuu wa Simba , Patrick Aussems kuachana na Simba kulikuwa na taarifa kuwa alikuwa na mawasiliano na klabu ya Polokwane City ya Afrika Kusini.
Inadaiwa moja ya sababu ya Simba kuachana na Patrick Aussems ni yeye kwenda Afrika Kusini kwa ajili ya kufanya mazungumzo ya kuifundisha Polokwane City.
Na taarifa zinadai kuwa Patrick Aussems alifikia makubaliano na Polokwane City ya kuifundisha. Na kocha huyo ambaye aliipa mafanikio Simba msimu jana kwa kuifikisha robo fainali ya ligi ya mabingwa barani alipanga kuondoka na Jonas Mkude pamoja na Chama.
Lakini kwa Habari za ndani , Polokwane City wamesitisha mpango wao wa kuwa na kocha huyo kutoka Ubelgiji. Kwa maana hiyo yeye pamoja na wachezaji kama Jonas Mkude na Chama ambao walikuwa kwenye mipango yake ya kwenda nao basi mpango huo umekwama.