Sambaza....

Mechi za mkondo wa kwanza za nusu fainali ligi ya mabingwa zinaanza usiku wa jumanne hii tarehe 26/04/22 kwa mchezo moja tu.
Man City wakiwa nyumbani wanawakaribisha Real Madrid kutoka Uhispania, mechi inayotazamiwa kuwa na ushindani wa juu sana kutokana na ubora wa timu zote mbili.

Uzoefu wa mabenchi ya ufundi Real wakiongozwa na mkongwe Carlo Ancelotti huku City wakiongozwa na Pep Guardiola kocha kijana mwenye maarifa mengi na historia nzuri ya kutwaa kombe hili.

Ancelotti ametwaa kombe hili mara 1 akiwa kocha wa Real Madrid msimu wa 2013/14 huku Guardiola akitwaa ubingwa mara mbili akiwa na Barcelona 2008/09 na 2010/11.

Carlo Ancheloti kocha wa Real Madrid.

Time zote mbili zina wachezaji wazuri, nathubutu kusema “World Class Players” daraja A kabisa na hii ndiyo inanipa kiburi kwamba mechi itakuwa na upinzani wa juu sana kutokana na aina ya wachezaji watakao husika.

Makocha wote wanatumia mfumo wa 4-3-3 wakijivunia idara zao za viungo kwa mfano City pale ndipo utakapo waona akina   Riyad Maharz, Bernardo Silva, Kevin De Bruyne na upande wa Real wakiwa na ‘utatu wao mtakatifu’ wa viungo wazoefu Luka Modric, Toni Kroos, Casemiro.

Niachie hapo kwenye utamu unaoweza kupatikana kwenye idara ya kiungo, baina ya wakongwe na machipukizi wakipambana kupata matokeo.

Pep Guardiola kocha wa Manchester City.

Mechi hii ina sura kubwa ya kivita vya Kijiografia, ukiacha Wahispania vs Waingereza kutokana na asili ya hizi timu, lakini kuna jambo jingine la ziada Wabrazili kuingilia hivi vita.

City ina wachezaji kadhaa toka taifa la Brazil akiwemo golikipa Ederson, Gabriel Jesus na Fernandinho. 

Huku Real wakiwa na Vinicius Jr, Elder Militoa, Casemiro na Rodrygo ambao wamewaka wako kwenye kiwango bora kabisa kwa sasa, kama ambayo Jesus wa City akiwa kwenye kiwango bora sana.

Kiungo wa Real Madrid Luca Modric.

Mkongwe Luka Modric ‘kisu cha mgema kinachozeeka na makali yake’ yupo kwenye form ya hatari akishiriki kwa kina kwenye mafanikio ya Real hadi kufikia hapa ilipo sasa.

Benzema kama De Bruyne sina kumbukumbu kuwa “out of form” kwao ilikuwa lini tangu wamekiwasha. Kwasasa huwezi kuitaja Real kama hutamtaja Karim Benzema ambaye Wafaransa wanamuita ‘Benzizziou ‘ wakiwa na maana ya mfalme.

Kevin De Bruyne kiungo wa Manchester City.

Lakini kwenye lango pale golini pande zote mbili zina watu wa maana sana Thibaut Courtous na Ederson si wa mchezo mchezo hata kidogo, kwa kweli tungoje game nzuri ya kiufundi.

Makocha hao pia wanajivunia wachezaji watakao tokea nje kuja kusahihisha kilichokosekana kwa watangulizi wao mtu kama Camavinga kwa upande wa Real huwa anaingia na jambo sawa kabisa na Grealish kwa upande wa City.

Na matumaini macho yetu hayata boreka kwa mchezo huu. Itakua ni  “Classic Game”.

Sambaza....