Baada ya michezo yote ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika kumalizika na kutoa timu nane zitakazoshiriki hatua ya robo fainali sasa droo ya robo fainali ya michuano hiyo inasubiriwa kwa hamu.
Kama kawaida vinara wa kila kundi watakuna na timu zilishika nafasi ya pili lakini pia wataanzia mechi zao ugenini na kumalizia nyumbani. Yanga wao pia ni vinara katika kundi lao hivyo wanapata faida hiyo pia.
Vilabu vya Afrika Kasakazini kama ilivyo ada vimeendelea kuonyesha ubabe wao kwani kati ya vilabu nane vilivyofuzu nusu ni kutoka katika nchi za Kiarabu. Huku nafasi hizo nne nyingine wakigawana maneneo mengine ya Afrika.
Yanga baada ya kumaliza kinara katika kundi lake huenda akakutana na Rivers United (Nigeria), Pyramdis (Misri) au USM Alger kutoka Algeria waliomaliza katika nafasi ya pili. Wababe wengine waliomamiza katika nafasi ya kwanza ni Asec Mimosa (Ivory Coast), Marumo Gallants (Afrika Kusini) na AS FAR ya Morocco.
Droo ya michuano hiyo ya Shirikisho Afrika pamoja na Ligi ya Mabingwa Afrika zitafanyika nchini Misri April tano mwaka huu ambapo zitakua mubashara kupitia televisheni pia.
Baada ya kumaliza majukumu hayo ya Kimataifa sasa Yanga wanarudi nyumbani na wataanza na kibarua cha michuano ya FA dhidi ya Geita Gold halafu watakutana na Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu.