Sambaza....

MSHAMBULIZI, Amis Tambwe ‘Mr.Hat Trick’ amerejea. Ndiyo amerejea baada ya miezi 14 ya mateso raia huyo wa Burundi amefanikiwa kuipa Yanga SC ushindi wa kuvutia dhidi ya Singida United jana Jumapili na kuipeleka timu yake hiyo kileleni mwa msimamo.

Tambwe alifunga magoli yote mawili, la kwanza kwa kichwa akiunganisha mpira mrefu wa krosi uliopigwa na mlinzi wa kushoto Gadiel Michael nusu saa baada ya kuanza kwa mchezo. Lilikuwa goli la stahili yake kiufungaji, hata lile la pili alilofunga katika dakika ya mwisho ya nyongeza katika kipindi cha kwanza akiwa ndani ya eneo la hatari limeonyesha namna mfungaji huyo aliyekuwa katika majeraha mfululizo namna alivyo fiti kimwili na akili.

Aligusa mpira kwa mguu wa kulia na wakati mabeki wakijiandaa kuweka miguu yao kuzuia, kwa kitendo cha haraka ‘touch’ yake ya pili katika mpira ilikuwa ni kushuti vizuri golini na alifunga goli ambalo siku zote washambuliaji makini ufunga. Magoli hayo mawili ni salamu tosha kuelekea upande wa mahasimu wao Simba SC wakakaokutana Jumapili ya wiki hii katika mchezo wa kwanza baina yao katika ligi.

Ikumbukwe, Tambwe kiujumla tayari amefunga magoli matano katika michezo ya ‘Dar es Salaam-Pacha’-magoli matatu akifunga mara tatu mfululizo katika michezo mitatu ya ligi kuu dhidi ya Simba. Mara mbili aliifunga Yanga AKIWA mchezaji wa Simba katika mchezo wa Nani Mtani Jembe 2013.

Image result for hamis tambwe

Namna Tambwe alivyofunga, uso wake wakati anashangilia mabao yake, makofi aliyojibu baada ya mashabiki wa klabu yake kuanza kumshangilia kwa nguvu uku wakimpigia makofi wakati akitoka uwanjani na ufiti aliouonyesha kwa robo tatu yote ya mchezo alipokuwepo uwanjani ni dhahiri yupo fiti kuanza katika pambano lijalo vs Simba.

Heriter Makambo ambaye tayari amefunga magoli mawili katika michezo mitatu aliyoichezea Yanga katika ligi kuu, Mrisho Ngassa mwenye goli moja na pasi moja ya goli wote hawa walipumzishwa kusubiri mchezo wa Jumapili na kwa hakika kocha Zahera Mwinyi atakuwa ameungana na mashabiki wake wengi kujipa matumaini kutokana na kiwango kilichoonyeshwa na Matheo Anthony na Tambwe katika pambano dhidi ya Singida United.

Kufunga kila mchezo kati ya minne waliyokwishacheza kunaifanya ‘Timu ya Wanachi’ kushinda ushindi wa asilimia 100 na kujikita kileleni mwa msimamo. Waliifunga Mtibwa 2-1 na ushindi wa jana dhidi ya Sindiga United unaifanya Yanga kupata ushindi dhidi ya timu ambazo walishindwa kuzifunga msimu uliopita, Simba pia walikuwa katika kundi hilo, watapona? Tambwe karudi, Makambo, Ngassa watakuwepo!

Sambaza....