Sambaza....

Katika muendelezo wa story na beki mahiri wa “Kino Boys” KMC Ally Ramadhani maarufu mtaani kwao kama “Kibampani” leo anatuelezea ni jinsi gani alikaribia kuachana na mchezo pendwa wa Kandanda kutokana na changamoto ya kukatwa katika timu.

Ally Ramadhani anasema anakumbuka ilikua katika kipindi cha michuano ya Copa Cocacola ambapo alifika mpaka hatua ya mwisho ya uchaguzi lakini jina lake likakatwa mwishoni kabisa anasimulia mchezaji huyo aliepitia katika Academy ya Champion Kawe.

Ally Ramadhani Oviedo akiwafungisha tela wachezaji wa Yanga.

Oviedo ” Nakumbuka nilikua na timu ya mkoa wa Kinondoni (Mkoa wa kisoka), sasa pale kulikua na mchujo wa kwenda kuunda timu ya Kitaifa. Nilikua vizuri wakati ule, nilikua fiti sana na niliamini nafasi ilikua yangu lakini walikuja kuchaguliwa watu wengine ambao naamini walikua hawaniwezi kabisa katika nafasi yangu.

Iliniuma sana mpaka nikataka kuachana na mchezo wenyewe, sikuona tena sababu ya kuendelea na mpira. Lakini mambo yanabadilika na maisha yanaenda leo hii nipo KMC”

Ally Ramadhani akiwa na wachezaji wenzake wakimsikiliza kocha kwa makini.

Oviedo ambae amedumu  kwa misimu minne na klabu ya soka ya KMC  aliyojiunga nayo akitokea klabu ya Changanyikeni Rangers iliyokua inashiriki Ligi daraja la pili ngazi ya Taifa.

Ni miongoni mwa wachezaji wachache waliobaki na timu tangu KMC ipande Ligi kuu kutokana na wengi wao wengine kuachwa. Yeye (Oviedo) na Reyman Mgungila ndie wachezaji waliodumu kwa muda mrefu na KMC, tangu timu ipo daraja la kwanza.

 

 

Sambaza....