Muda umepita tangu aliyekuwa kocha wa klabu ya Yanga Mwinyi Zahera kufukuzwa na klabu ya Yanga. Klabu ambayo awali alijenga urafiki ambao ulionekana kufikia hatua ya hatua ya undugu.
Lakini Baada ya kufungwa na Pyramid FC kwenye mechi ya kombe la shirikisho barani Afrika na kutolewa kwenye michuano hiyo klabu ya Yanga ilimfukuza kocha huyo.
Pyramid FC ilikuwa inaongozwa na kocha mkuu Sebastien Desabre , kocha huyo naye amefukuzwa rasmi kwenye klabu hiyo Baada ya mfululizo wa matokeo mabovu ndani ya kikosi hicho.
Sebastian Desabre ameiacha Pyramid FC katika nafasi ya saba (7) ikiwa na alama kumi na mbili (12) katika michezo nane (8) .
Sebastian Desabre ameiongoza Pyramid FC katika mechi kumi na tisa (19) na kushinda mechi kumi na mbili (12) alitoka sare mechi nne (4) huku akifungwa mechi tatu (3). Mara ya mwisho kupata ushindi ilikuwa Oktoba walipoifunga El-Harby magoli (3-2). Kocha wa zamani Al Ahly , Abdel Aziz Baden Shafy amechaguliwa kocha mpya wa Pyramid FC.