Tumeona mara nyingi wachezaji wa kandanda kwa furaha baada ya mechi kumalizika hutupa zawadi kwa mashabiki wao. Wapo ambao hutoka uwanjani wakiwa na nguo za ndani tu, Neymar na Buffon ni moja kati ya wachezaji magalacha ambao wamewahi kufanya hivyo. Kwa furaha zao wangeweza hadi kuvua nguo za ndani na kuwapa mashabiki wao, lakini wangevaa wapi?? hahaaa.
-Buffon
Wiki iliyopita kulikuwa na mchezo wa Ngao ya Jamii, hakukuwa na mtu aliyevua bukta na kubaki na nguo ya ndani, wala kocha wa Azam Fc, Etiene Ndayiragije , hakugawa medali yake kwa shabiki mtoto wa Simba kama alivyofanya Jose Mourinho miaka kadhaa katika fainali ya Ngao ya Jamii huko Uingereza pale Man Utd ilipopoteza mbele ya Arsenal Fc. Lakini, matokeo yalikuwa mazuri kwa upande wa klabu ya Simba Sc na furaha hiyo ilionyeshwa zaidi na Mo Dewji, shabiki na mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya klabu hiyo.
Furaha ya Mo ilimpelekea kuvua tai yake ya rangi ya kijivu na kuitupa upande walipokuwa mashabiki wa Simba Sc sehemu ya VIP B. Kama ilivyo kawaida, mashabiki hao waliing’ang’ania tai hiyo ambayo kwa mujibu wa mtandao wa gentlemensguru tai bora zaidi 2019 inaweza kuwa kati ya dola 40 au 80 (92,000 au 184,000 Tzs) na kwa hadhi ya Mo inaweza kuwa zaidi ya dola 220 (506,000 Tzs) bila shaka kuna mmoja aliondoka nayo.
-Mo Dewj kabla ya kuvua tai
Tai ya kijivu kwa mujibu wa wataalamu wa rangi za tai inaonyesha kuwa mvaaji ni hana usawa, mhafidhina na katengwa. Bila kujali maana pia tai za rangi ya kijivu huonyesha mtu mwenye uweledi, rasmi na fahari.
Jamaa aliyepata tai hii anaweza kuivaa katika sherehe hata kama kuna mtoko ‘amaizing’ bila kusahau hata katika ‘interview’ ya kazi, ofisni, au mkutano wa kibiashara lakini kumbuka maana kwa watu ambao watakuchambua kwa mavazi yako. Zaidi anaweza iwekea katika flemu ya ukutani kama kumbukumbu ya zawadi kutoka kwa Mo Dewji moja ya matajiri wakubwa barani Afrika.
Kwa upande wa Mo hii kwake inaweza kuwa ilikuwa zawadi kubwa kwake achana na kile anachoifanyia klabu hiyo kama shabiki na muwekezaji, angeweza hata pia kutoa koti la suti au saa yake pia, pasingetosha pale. Hakika ni shabiki wa nguvu wa Simba Sc