Msemaji wa klabu ya Yanga Ali Kamwe amewaita Wananchi kuelekea mchezo wao wa pili wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya TP Mazembe utakaopigwa siku ya Jumapili February 19 katika Dimba la Benjamin Mkapa.
Yanga inakwenda kutupa karata yake ya pili katika michuano hiyo baada ya mchezo wa kwanza kupoteza mabao mawili kwa sifuri ugenini dhidi ya US Monastir Tunisia.
“Kwa ukubwa tulionao Tanzania na kwa ukubwa tulionao Yanga lazima tukawaonyeshe Afrika kwamba sisi ni wakubwa sio tu ndani hata nje ya uwanja. Lazima twende tukajae pale uwanjani tuwaonyeshe TP Mazembe sisi ni nani,” Ali Kamwe msemaji wa klabu ya Yanga.
Kamwe pia aliwatangazia mashabiki wa klabu ya Yanga kujitokeza kwa wingi katika shughuli ya uhamasishaji kuelekea mchezo huo zitakazofanyika Mbagala Zhakiem leo hii.
“Umoja wa matawi ya wilaya ya Temeke wameandaa shughuli yao pale Zhakiem (Mbagala) ya uhamasishaji kuelekea mchezo wetu wa Jumapili.
Mimi kama msemaji niliwaambia lazima tutengeneze “connection” kati ya wachezaji na mashabiki hivyo nitahakikisha wachezaji wa Yanga watakuepo pale na kuwaelezea wenyewe mashabiki wamejiandaaje na mchezo wa Mazembe,” Ali Kamwe.
Yanga ina kila sababu yakushinda mchezo huo wapili katika kundi lao ili kuweka matumaini yao hai yakuelekea robo fainali.