Kuelekea mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kati ya Yanga na USM Algier Klabu ya Yanga imekuja na kauli mbiu itakayotumika katika mchezo huo wa kihistoria.
Akizungumza mbele ya Waandishi wa habari Afisa habari wa Klabu ya Yanga Alli Kamwe sambamba na kutangaza kauli mbiu ya mchezo huo lakini pia amesema ni kwa kiasi gani wamepata tabu kuchagua kauli mbiu hiyo.
“Tumepata shida sana katika kuchangua “slogan” ya mchezo huu kwasisi viongozi kila mtu alikua na shauku na mchezo huu, tuliwashirikia mashabiki wetu ili kila mtu atoe maoni ni slogan ipi itimie na tulipata maoni zaidi ya 6000,” alisema Kamwe na kuongeza
“Kwa Klabu ya Yanga huu ndio umekua mwaka wakwanza tumefika fainali za Afrika na klabu hii ina miaka 80, hivyo viongozi wana hamu yakuvaa medali na majina yao yaandikwe katika vitabu vya historia.
Miaka 30 imepita tangu nchi hii ikaribie kubeba kombe la Afrika, mara ya mwisho ilikua ni 1993 sasa fikiria nchi imekaa muda wote huo bila kufika fainali. Lakini si tu Tanzania pia nchi za Kenya, Burundi na Uganda nao wamekiri sisi ndio watetezi wao katika michuano hii ya Afrika.”
Ni rasmo sasa Alli Kamwe ametangaza kauli mbiu itakayotumika katika mchezo huo ambapo fainali hizo zitapigwa mara mbili May 28 Benjamin Mkapa na June 4 nchini Algeria.
“Why not us?”, Kwanini sio sisi?, hii ndio itakua slogani yetu yaani Kwanini sio sisi Yanga, kwasisi sio sisi Tanzania, kwanini sio sisi Afrika Mashariki?,” alisema Kamwe.
Sambamba na kauli mbiu hiyo Alli Kamwe alitangaza viingilio ambavyo vitatumika katika mchezo huo wa kihistoria utakaopigwa siku ya May 28 Jumapili saa kumi jioni.
Alli Kamwe “viingilio vitakua kama ifuatavyo
Royal (jezi za ubingwa, usafiri, chakula) 200,000, VIP A ni 100,000, VIP B itakua ni 30,000
na VIP C ni 15,000 wakati mzunguko itakua ni kwa 5,000 pekee.”