Sambaza....

TANGU kuwasili kwake Tanzania, Amis Tambwe amefunga magoli mengi zaidi dhidi ya Mbeya City FC kuliko timu nyingine yoyote katika ligi kuu na mshambulizi huyo wa Kimataifa wa Burundi jioni ya Leo atakuwa akitafuta goli lake la kumi vs timu hiyo ya Manispaa ya Mbeya.

City wanaikaribisha Yanga katika uwanja wa Sokoine, Mbeya katika muendelezo wa michezo ya ligi kuu Tanzania Bara na lazima wamchunge Tambwe aliye katika kiwango cha juu.

Mshambulizi huyo wa zamani wa timu ya Taifa ya Burundi amefunga magoli matano katika michezo mitatu iliyopita ya timu yake katika michuano yote – ikiwemo Hat Trick dhidi ya Tukuyu Stars ya Mbeya katika kombe la FA mapema wiki hii.

Taarifa

Tarehe Muda Ligi Msimu Mwisho
29/12/2018 4:00 pm TPL 2018-2019 90'

” Haijalishi kama nitafunga ama sitafunga, jambo kubwa tunataka kushinda kama timu na simchezaji mmoja mmoja.” anasema Tambwe nilipofanya naye mahojiano mafupi Ijumaa hii akiwa Mbeya.

” Tunahitaji ushindi katika mchezo dhidi ya Mbeya City, yeyote atakayefunga ni faida kwa timu lakini kama ilivyo kwa washambuliaji wengi, nitafurahi kama ilivyo kwa washambuliaji, kufunga ni hitaji la kwanza ukiwa mchezoni.” anasema Tambwe ambaye tayari amefunga mara tisa dhidi ya timu hiyo ya Mbeya.

Alifunga mara tano mfululizo, yakiwemo magoli matatu aliyofunga katika msimu wake wa kwanza Bara akiwa mchezaji wa Simba SC na magoli mengine sita akiitumikia timu yake ya sasa Yanga-ikiwemo Hat Trick msimu wa 2014/15.

” Huwa sitazami nafunga dhidi ya timu gani. Kikubwa tunaomba sapoti na mshikamano wa mashabiki wetu uendelee kuwa nyuma yetu hatutawaangusha.”

Sambaza....