Katibu wa Baraza la Wazee wa Yanga SC, Ibrahim Akilimali, ameweka wazi kuwa baadhi ya wachezaji walioshindwa kusafiri na timu kuelekea Algeria hapo jana kwa kusema kuwa wanaidai klabu hiyo
Kikosi cha Yanga SC, kiliondoka jana Alasiri kuelekea Algeria kwa ajili ya mchezo wa mzunguuko wa kwanza wa hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho dhidi ya USM Alger
Akilimali amesema kuwa, wachezaji waliobaki hawajabaki bila sababu na baadala yake wanaidai klabu hiyo ndio maana wameshindwa kusafiri na timu
Katibu huyo, alienda mbali zaidi kwa kusema yeye hataki kuwa mnafiki na msema kweli siku zote ni mpenzi wa mungu
Wachezaji waliobaki nchini ukiondoa waliomajeruhi ni Kelvin Yondan, Papy Tshishimbi, Obrey Chirwa na Ibrahim Ajibu Migomba
Yanga SC, inataraji kushuka dimbani kuwavaa USM Alger siku ya Jumapili Mei 6, 2018