Sambaza....

Klabu ya soka ya Yanga jana mchana imeondoka kuelekea Algeria tayari kabisa kwa mchezo wao wa kwanza wa hatua ya makundi ya Kombe La Shirikisho Africa dhidi ya USM Algiers.

Kikosi hicho kimeondoka jana jioni katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere na kupitia Dubai kabla ya kupanda tena ndege kuelekea Algeria.

Yanga imeondoka ikiwa bila ya wachezaji wake muhimu haswa wa kigeni. Mchezaji pekee wa kigeni alieondoka na timu ni Youth Rostand raia wa Cameroon, huku Obrey Chirwa, Thaban Kamusoko hawakuambatana na timu, Donald Ngoma na Hamis Tambwe wakiwa majeruhi wa muda mrefu. Pia kiungo wake Papy Tshishimbi haikuweza kufahamika kwanini hakuambatana na timu katika mchezo huo muhimu.

Sio hao tuu lakini wachezaji muhimu wazawa wa Yanga nao hawakusafiri na timu jana. Manahodha wote wawili  Nadir Haroub na Kelvin Yondani hawajasafiri na timu hivyo kuifanya Yanga kukosa nahodha katika mchezo huo.

Pia mshambuliaji wao fundi Ibrahim Ajibu amebaki Tanzânia na kukosa mchezo huo wa kwanza wa hatua ya makundi na kuifanya timu ya Yanga kuondoka na wachezaji 18 pekee.

Wachezaji wa Yanga waliondoka na timu ni Youthe Rostand, Ramadhan Kabwili, Hassan Kessy, Andrew Vincent, Haji Mwinyi, Gadiel Michael, Pato Ngonyani, Said Makapu, Juma Abdul, Yussuf Mhilu, Mwashiuya Geoffrey, Pius Buswita, Rafael Daud, Yohana Nkomola, Emmanuel Martin, Juma Mahadhi, Abdallah Shaibu na Said Makapu.

Sambaza....